Header Ads

Header ADS

Waandishi wa habari wapewa mafunzo ya kuripoti habari.

    Christophe Legay ambaye ni  Mratibu wa Mradi wa SDC kutoka UNESCO,akizungumza pindi akifungua mkutano wa mafunzo ya Waandishi wa Redio jamii 25 jinsi ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO lakini pia mafunzo hayo yatachukua muda wa siku 5 ambapo yanafanyikia katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo,chini ya  udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC).











 Katika mafunzo hayo ambayo Waandishi kutoka kanda mbalimbali nchi ambao wanahudumu katika Redio jamii  wameudhuria mafunzo hayo ya siku 5 mjini hapa kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine.
    Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) washiriki watajifunza namna ya kuripoti maafa na pia mfumo wa kitaifa wa kukabiliana na majanga.
Akizungumza mjini hapa Christophe Legay, Mratibu wa Mradi wa SDC kutoka UNESCO amesema kwamba kutokana na kuongezeka kwa majanga na uelewa duni wa wananchi, UNESCO imeona vyema kufunza wanahabari  kwa dhumuni la kuweza kuelimisha jamii inayowazunguka.                                                              











Aidha,alieleza kuwa hayo ni mafunzo ya tatu ya waandishi wa habari pia imesaidia kwa wale ambao hawakuwai kupata mafunzo hayo.
Hata hivyo, Legay alisema kwamba   majanga ya asili yamekuwa yakijitokeza sana na kwa kasi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi  hivyo  imeonekana haja ya kuwapatia wananchi mafunzo maalumu ya kukabiliana na majanga hayo ikiwa na pamoja na kujiweka tayari.
"Tunataka wananchi watambue namna ya kukabiliana nayo majanga hayo, ili kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa jamii ambayo wanaitumikia" alisema Legay na kuongeza kuwa wanapowanoa waandishi wamelenga kuwawezesha kuwa na namna bora ya kuandika habari za majanga ili kusaidia kuokoa na kujipanga lisitokee tena.
Aidha,Lwgay ameeleza kuwa Waandishi wengi kwa sasa jindi ya uandika hairidhishi na hivyo kuchochea zaidi hasara badala ya kukabiliana na dhiki hiyo na kuokoa maisha na mali.
Legay alisema watu wakitambua namna ya kusimamia maafa na matumizi ya raslimali na nyenzo za usimamizi hasara kwa mali na watu zitapungua.

Alisema pamoja na majanga ya asili yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, pia kuna majanga yanayosababishwa na shughuli za binadamu kama vile milipuko ya matanki, ajali mbalimbali ambazo wananchi amekuwa wakijihudumia badala ya kuokoa mali na watu.
Kwa upande wake mtaalamu wa sayansi asilia kutoka UNESCO ambaye ni Kevin Robert  alisema ni wajibu wa waandishi wa habari kwanza kutambua namna ya kukabiliana na majanga, elimu ambayo itawapa undani wa nini kinatokea, wafanye nini na nani asaidie wawe na taarifa sahihi za kusaidia wananchi.

Robert alisema wanahabari hao kutoka Redio 25 na Mratibu kutoka mtandao wa Redio za Jamii zilizotawanyika nchini kote ikiwamo mikoa ya Lindi,Katavi, Kilimanjaro Mara wanafundishwa mifumo ya upashanaji habari katika maafa, mifumo ya habari, kitengo cha maafa na utaratibvu wake na namna nzuri ya kusaidia waliokumbwa na mafaa.

Tanzania kwa sasa imeshakabiliwa na majanga ya asili mengi kama  mafuriko, ukame, upepo mkali, tsunami, mmomonyoko wa bahari,  mvua za mawe na upepo mkali  kama wa Kahama na mafuriko ya Mtwara, 2015 na pia kulipuka kwa lori la mafuta mjini Morogoro.
Katika ajali ya Morogoro wananchi badala ya kuokoa walikuwa wanaiba mafuta hadi lori lilipolipuka.
Aidha,Robert aliwataka Waandishi hao kuelewa Sheria ya Uratibu wa Misaada ya Maafa Namba 9 ya 1990 (iliyofutwa na Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya 2015) na kujua kazi ya kitengo cha Kuratibu Misaada ya Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na kutambua changamoto zilizopo.
Lakini pia,alieleza lengo kubwa na mategemeo ya UNESCO ni kuitaji kuona kuwa kutokana na mafunzo hayo yanaleta mabadiliko makubwa katika upashanaji wa habari vilevile katika kukabiliana na majanga pamoja na maafa nchini.

No comments

Powered by Blogger.