Header Ads

Header ADS

Serikali ya Tanzania inatarajia kupata Dola milioni 500 za Kimarekani.

   Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye ni Waziri wa fedha na mipango amefanya mazungumzo na Bi. Anne Namara Kabagambe ambae ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Benki ya Dunia anayewakilisha nchi za Afrika huko Mjini Washington DC, Marekani.
      Lengo kuu la mazungumzo hayo yalikuwa kubadilishana uzoefu juu ya utekelezaji wa Sera mbalimbali za fedha na namna uchumi wa Dunia unavyoendeshwa.
  Aidha,Katika mazungumzo hayo baadhi ya miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa(SGR), ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha umeme la mto Rufiji, mradi wa elimu,na miradi ya mfuko wa maendeleo ya jamii(TASAF) ilizungumziwa.















   lakini pia,Dr. Mpango alieleza dhamira ya Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuinua kiwango cha elimu, kwa kutafuta fedha zaidi na mikopo ya masharti nafuu ambayo itaelekezwa kwenye elimu.
    ‘’Katika Mradi wa Elimu unaotarajiwa kuwasilishwa Benki ya Dunia mwezi Novemba, 2019, tunatarajia kupata dola za Marekani milioni 500, na nimemuomba Bi. Anne Namara Kabagambe azidi kusisitiza ili Taifa liweze kupatafedha hizi kwa wakati, na tunaamini kwamba fedha hizo zitaidhinishwa na Benki ya Dunia kama tunavyotarajia.”Alisisitiza Dkt Mpango.
   Aidha,Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango alisema pamoja na miradi ya Elimu, Sekta ya nishati ya umeme pia ni muhimu katika kuinua uchumi wa nchi kwa sababu ukipatikana umeme wa kutosha utasaidia kwa vitendo agenda ya uchumi wa viwanda kwa kuongeza thamani ya mazao na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii nchini.
    Aliiomba Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa zisaidie kwenye miradi ya mikubwa inayotekelezwa na Serikali hasa katika sekta ya umeme na miundombinu.
   Lakini pia, Dkt. Mpango alieleza kuwa hivi karibunii Benki ya Dunia iliipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 450 kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF, awamu ya tatu.















    “Hivyo kupitia miradi miwili ya Elimu na TASAF, Tanzania inatarajia kupata dola za Marekani milioni 950”. Aliongeza Dkt. Mpango
     Lakini pia,Kwa upande wa Benki ya Dunia Bi. Anne Namara Kabagambe alielezea kufurahishwa na utekelezaji wa miradi inayofanyika Tanzania kwani alipata fursa ya kuona miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na miradi inayotekelezwa na TASAF, na kuelezea kuwa ni miradi ya mfano na kwa nafasi yake ataendelea kuitangaza miradi hiyo ili Tanzania iweze kupata fedha zaidi ya kutekeleza miradi hiyo.
    Dkt. Mpango anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Dunia IMF ambapo amesema mikutano hiyo ni muhimu kwa kuwa nchi itapata fursa ya kuweza kujadiliana na Taasisi hizi za IMF na WB kuhusu miradi wanayofadhili.
    Aidha, kupitia mikutano hiyo vipaumbele vya nchi vitaelezwa na kupitia changamoto zilizopo kwa sasa, kutetea maslahi mapana ya Tanzania katika utekelezaji wa programu za maendeleo na mabadiliko ya kimfumo katika uendeshaji wa uchumi kutegemeana na mwenendo wa Dunia unavyokwenda.
    Lakini pia,ameeleza kutoka na nchi nyingine  wanavyotekeleza na kusimamia program zao  ndivo na Tanzania inavopata uzoefu lakini hata hivyo Tanzania iavozidi kutekeleza program mbalimbali za kimaendeleo pia nchi zingine kutambua jambo hilo.
     Imeripotiwa na Mwandishi;Adolf Mwingira

No comments

Powered by Blogger.