Header Ads

Header ADS

Serikali yataka Mtambo wa Hale urejee katika hali yake ya mwanzo.

     Dkt.Medard Kalemani ambaye ni Waziri wa nishati ameeleza mpango wa Serikali ni kutaka kurudisha hali ya mtambo wa umeme hale unakuwa katika hali yake ya mwanzo ili uweze kufanikiwa katika kutoa megawatts 21 kama ilivyosanifiwa na kuanza kufanya kazi mwaka 1964.
    Hayo ameeleza wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme cha Hale wilayani Korogwe mkoani Tanga ambapo pia alitembelea mgodi wa kufua umeme.
      Waziri Kalemani akiwa katika kituo hicho alisema kwamba ametembelea mradi huo kwenye maeneo makubwa mawili ya mashine na trasfoma huku akieleza kwamba kwenye mashine mbili ambazo zipo eneo hilo hazifanyi kazi kwa sasa maanake hatupati megawati hata moja kutoka kwenye mtambo huo.













Aidha ameeleza kwamba ingawa mtambo mmoja unafanyiwa marekebisho kwa maana ya kufungwa vifaa na wataalamu hivyo watahakikisha unakamilika na tayari alikwisha kutoa maekelezo kazi hiyo ikamilike ili megawatts 10.5 zirejee.
        “Hapa katikati mlikuwa mnapata megawatts 8 zilikuwa hazifiki hata kumi ..wakati huu matengenezo makubwa yanafanyika hivyo ni matumaini yake kwamba hata mkandarasi ambaye anatafutwa kwa ajili ya kufanya matengenezo ya mitambo yote miwili utafanyika haraka “Alisema Dkt Kalemani 
      Hata hivyo alisema lazima wahakikisha wanakuwa na umeme wa kutosha ambao utapatikana kwenye mradi huo ambao ni wa miaka mingi kwani ulijengwa mwaka 1964 hiyo mitambo kila wakati lazima ifanyiwe ukarabati hasa wakati unapopita.
   “Mwaka juzi nilipita hapa na kutoa maekelezo kutokana na kuwepo dalil za mitambo iliyochakaa nikawaambia muanze utaratibu wa kufanya marekebisho ya mitambo yote wakati wa ziara yangu kupita kwenye mitambo ni kujihakikisha umeme unapatikana na wa uhakika”Alisema
       Lakini pia,Mwanzo akizingumza wakati wa ziara hiyo Jacline Mtolela ambaye ni Mhandisi Mkuu wa kituo cha kuzalishia umeme cha  Pangani Hydro System  alimueleza Waziri Kalemani kwamba hali ya mitambo iliyopo kwnye kituo hicho ni chakavu ya mwaka 1964ina hitaji matengenezo makubwa.
     Aidha, ameeleza kwamba kwa sasa wapo kwenye mpango wa kutafuta Wakandarasi kwa ajiri ya kukarabati kwani kwa sasa wana uwezo wa kuzalisha megawatts 10.5 kwa mashine moja ila kutokana na uchakavu wa mashine wanazalisha megawatts 8 lakini mashine ipo kwenye matengenezo.
   

No comments

Powered by Blogger.