Serikali yamtaka Wakala wa Huduma Za Misitu Kupima Shamba La Miti La Rubya Ukerewe.
Dkt.Angeline Mabula ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi amemuagiza Wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kuhakikisha inalipima na kupatiwa hati shamba lake la Miti la Rubya lenye ukubwa wa hekta 1,926.3 lililopo kijiji cha Bugula tarafa ya Ilangala kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Hayo ameongea wakati akiwa kwenye ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakati akiwa katika ziara yake ya siku moja katika kisiwa cha Ukerewe kufuatilia utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika hamashauri za mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Aidha,ameeleza kwamba kwa sasa Wakala huyo anaitajika kuhakikisha shamba hilo la Miti la Rubya linapimwa na kupatiwa hati itakayoonesha mipaka halisi ya shamba hilo ili kuepuka migogoro ya ardhi.
‘’Miji inakuwa kuwa na wananchi bado wanahitaji maeneo bila kuwa na hati inaoonesha mipaka ya shamba kunaweza kuleta migogoro na tuelewe hati inalinda mipaka ya shamba lisivamiwe na wananchi’’ alisema Dokt Mabula
Lakini pia,Mabula ameagiza eneo la shamba kuwa Mpango Kina utakaonesha kila matumizi ya sehemu ya ardhi ya shamba hilo kwa kuwa katika eneo hilo mbali na shamba la misitu lakini kuna makazi ya watu.
Lakini kwa upande wa Festo Chaula ambaye ni Meneja wa Shamba la Miti la Rubya wilayani Ukerewe alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba an Maendeleo ya Makazi kuwa, Shamba la Miti la Rubya ni miongoni mwa mashamba 23 yanayomilikwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania lililoanzishwa mwaka 1951 kwa Tangazo la Serikali Namba 230.
Aidha,Alisema, pamoja na shamba hilo la Rubya pia Wakala inalo eneo lingine lilipandwa miti kwa ubia na halmashauri ya wilaya ya Ukerewe lenye ukubwa wa hekta 1,152 ambapo miti iliyopandwa eneo hilo ni ya Misindano.
Kwa mujibu wa Chaula, katika kuboresha makazi ya watumishi wa wakala wa Huduma za Misitu TFS katika mwaka huu wa fedha 2019/2020 TFS imetenga zaidi ya milioni 383.8 kwa ajii ya ujenzi wa nyumba tatu, tenki la kuhifadhia maji, ukarabati wa nyumba mbili na ujenzi wa uzio wa bustani ya miti ambapo ujenzi wa nyumba tatu ulianza Agosti mwaka huu.
Lakini pai,Katika Hatua Nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka halmashauri ya wilaya ya Ukerewe kufanya zoezi la upimaji maeneo katika halmashauri hiyo kama operesheni maalum ili kuondoa migogoro ya ardhi sambamba na kuondoa ujenzi holela.
Akizungumza na Madiwani pamoja na Watumishi wa Sekta ya Ardhi katika halmashauri hiyo, Dkt Mabula alisema tayari halmashauri hiyo inavyo vifaa vya upimaji inachotakiwa kwa sasa katika kuharakisha zoezi hilo ni kuwasiliana na Ofisi ya Ardhi Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kupatiwa Wapimaji.
Vilevile Dkt.Mabula alistaajabu sana kuona halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kutokuwa na kijiji chenye mpango wa matumizi bora ya ardhi wakati asilimia kumi ya kisiwa hicho ni ardhi ya nchi kavu. Halmashauri kerewe ina jumla ya vijiji 73 ambapo Naibu Waziri aliwataka Madiwani wa Halmashauri ya Ukerewe kuhakikisha inapanga mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji vyake ili kuainisha matumizi mbalimbali ya vijiji hivyo.
Lakini kwa upande wake George Nyamaha ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe alieleza sababu kubwa inayopelekea idara hiyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ni kutokana na upungufu wa Wataalamu wa sekta ya ardhi,hivyo basi imekuwa changamoto kubwa sana katika halimashauri yake.
No comments
Post a Comment