Header Ads

Header ADS

Serilaki yatoa agizo kwa waajili kuzingatia usalama wa wanfanyakazi wao.

   Jenista Mhagama ambae ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu,amewataka wamiliki wa maeneo ya kazi kuzingatia usalama na Afya mahali pa kazi kwa Wafanyakazi wao.
   Akizungumza katika hafla ya kufunga Mafunzo maalumu ya Usalama na Afya mahali pa Kazi kwa wakaguzi wa OSHA yaliyofanyika jijini Arusha, Mhe. Mhagama amesema kila ajira zinapozalishwa zinaenda sambamba na ajali pamoja na magonjwa, amesema hivyo waajiri wanapaswa kuhakikisha wanazingatia usalama wa wafanyakazi wao, amesema kukua kwa haraka kwa teknolojia inayotumika viwanda na maeneo mengine ya kazi kunagusa moja kwa moja afya na usalama wa wafanyakazi.













    Lakini pia  Bi Khadija Mwenda ambae ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA  amesema, walishirikiana na Shirika la Kimataifa la Workplace Health Without Borders (WHWB) katika mafunzo hayo kwa Wakaguzi, Khadija amesema Shirika hilo linalofanya kazi nchi mbalimbali dunia ikiwemo Tanzania pia limejenga uwezo kwa wakaguzi wa OSHA kuhusu masuala ya usalama na Afya, hivyo kupelekea na mabadiliko ya Teknolojia, amesema Shirika hiloa limetoa msaada wa vifaa mbalimbali ambavyo vitatumika kwaajili ya kufanya kaguzi mbalimbali meeno ya kazi.
     Kwa upande wao washirika wa Mafunzo hayo kutoka OSHA wameeleza kuwa Elimu waliyoipata wataitumia kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi, hususan kaguzi mbalimbali watakazokuwa wanazifanya.
    Imeripotiwa na Mwandishi wetu;Adolf Mwingira

No comments

Powered by Blogger.