TBS yapiga marufuku uuzaji wa vipodozi vyenye viambata vya sumu.
Maofisa wa Shirika La viwango Tanzania TBS wamefanya ukaguzi wa vipodozi kwa kushtukiza Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii ambapo wamepiga marufuku vipodozi vyote vyenye viambata vya sumu kwa kuwa vina madhara kwa watumiaji.
Ambapo vipodozi aina yote vilivyopigwa marufuku vimeondolewa sokoni maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza jijini Dar es Salaam.
Ambapo vipodozi aina yote vilivyopigwa marufuku vimeondolewa sokoni maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza jijini Dar es Salaam.
Maofisa shirika hilo walifanya ukaguzi huo mwishoni mwa wiki kwenye maduka mbalimbali yaliyopo Kariakoo.
Mhandisi Donald Manyama,Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi huo,Mkaguzi Mwandamizi wa Shirika hilo alisema wauzaji wa vipodozi hivyo wameonesha ushirikiano wa kutosha,kwani wamevitoa kwa kadri ambavyo walielekezwa.
Alipoulizwa kama kuingia nchini kwa vipodozi hivyo, kunachangiwa na kutokuwepo udhibiti wa kutosha mipakani,Mhandisi Manyama, alisema udhibiti upo wa kutosha,lakini vitu ambavyo vimepigwa marufuku nchini vinaingia kwa njia ambazo sio halali.
Alisema waingizaji wamekuwa wakitumia njia za panya kuingiza vipodozi hivyo. Alisema vipodozi walivyovikamata wamevichukua kwa ajili ya kwenda kuviharibu.
"Zoezi hili sio kwamba litaishia hapa (Dar es Salaam) baada ya kumaliza hapa tutaendelea na ratiba yetu mikoani kuondoa vipodozi hivi," alisema Mhandisi Manyama.
Alipoulizwa madhara ya vipodozi hivyo vyenye viambata sumu kwa matumizi ya binadamu,Manyama alisema vina madhara kwenye ngozi ya binadamu.
"Kwanza vinaichubua hiyo ngozi na kuifanya kuwa laini kiasi kwamba mtumiaji akifanyiwa operesheni ushonaji wake unakuwa ni mgumu," alisema na kuongeza;
"Vingine vinasababisha saratani ya ngozi, kupunguza kinga ya ngozi na kuathiri mfumo wa homoni za mwili. Hivyo tunawashauri hata watumiaji kuacha kutumia vipodozi hivyo. Wengine wanavitumia bila kufahamu, wakiona mwenzao amebadilika ngozi,wanadhani havina madhara.
Aidha,alieleza wataendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waache kutumia vipodozi hivyo.Alitoa wito kwa wasambazaji wa vipodozi hivyo kuacha, kwani wakikamatwa watawasababishia mitaji yao kupotea na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini.
Hata hivyo,alitoa wito kwa watumiaji kuacha kuvitumia kwa sababu ni hatari kwa afya zao. Baadhi ya vipodozi vilivyokamatwa kwenye ukaguzi huo na kuondolewa sokoni ni Carolight,Movate,Coco Pulp, Diproson,Viva White, Carotone, Bronz na Eclair.
Lakini pia vikiwemo na Citrolight, Tent Clear, Tender White, Clinic Clear, TCD, Baby Face,Light up,Dermotyl na Top Lemon. Mmoja wa wauzaji wa vipodozi hivyo, Rose Joseph, alishauri udhibiti uimarishwe zaidi mipakani,kwani kama vitaendelea kupatikana vitazidi kupata soko.
Vilevile mwisho alitoa pongezi kwa TBS kwa utendaji wao kazi wa kushtukiza kwani hatua hiyo inawasaidia kujua aina ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kutokana na kuwa na viambata sumu na kutoitajika kwa vipodozi hivyo katika masoko.
Imeripotiwa na Mwandishi wako;Adolf Mwingira
No comments
Post a Comment