Header Ads

Header ADS

Umoja Wa Ulaya Waongeza Tena Mda Wa Brexit

 Umoja wa Ulaya umekubali  kuchelewesha kwa muda wa miezi mitatu Uingereza kujitoa kutoka Umoja huo hadi Januari 31.

  Aidha,Kiasi siku tatu kabla ya tarehe ya mwisho ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya hapo Oktoba 31, mchakato wa Brexit bado haujulikani mwelekeo wake wakati wanasiasa wa Uingereza hawako karibu ya kufikia muafaka juu ya vipi, lini na hata iwapo hatua ya kuachana na Umoja wa Ulaya itawezekana.
  Hata hivyo,Mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya yamefikia makubaliano kuchelewesha Brexit hadi Januari 31, pamoja na uwezekano wa Uingereza kujitoa mapema iwapo bunge la Uingereza litaidhinisha makubaliano ya kujitoa Katika Umoja Huo.

No comments

Powered by Blogger.