Header Ads

Header ADS

Wananchi wa Kata ya Mavanga wilayani Ludewa Mkoani Njombe waungana kupiga vita mila potofu.

     katika kata ya Mavanga wilayani Ludewa mkoani Njombe,wananchi na Wakristu kutoka makanisa mbalimbali waungana kwa ajili ya kupeana semina ili kupiga vita mila potofu ambazo zimekuwa zikiendelea kufanywa na familia mbalimbali katika vijiji vya kata hiyo.
    Akizungumza katika kongamano lililowakutanisha wanaume wa kata hiyo mara baada ya kukamilika kwa kongamano la vijana na wanawake yaliyofanyika katika kanisa katoliki, Paroko wa parokia ya Mavanga  Padre Method Msanga amesema katika mazingira ya Mavanga kuna tatizo kubwa la imani potofu zinazopelekea watu kuchukiana.












    “Tatizo kubwa tuliloliona ni watu kukata tamaa hasa vijana kwasababu hawaioni imani ya Mungu na badala yake wanaiona imani hiyo nyingine ya mila potofu na ya kishirikina hivyo tunataka tuamshe mioyo ya watu tufuate imani ya kweli na mwishoni tusiwe na hofu yoyote wala woga kwasababu Mungu yupo na baadaye tupate maendeleo”alisema Padre Method  Msanga
   Kwa upande wake Mchungaji kanisa la Anglican Faraja mapunda  anasema wapo waumini wengi hawafiki makanisani kutokana na miungu mingine wanayoabudu kijijini hapo, kwa kuitolea sadaka wakiamini miungu hiyo inawasaidia kuwapa utajiri na wengine wakiamini inawaletea mvua kitu ambacho sio kweli.
  “Kwa mfano kwenye vijiji vyetu mtoto wa kiume ambaye ni wa kwanza kuzaliwa  wanasema lazima afanyiwe mila na wao wanaamini kwamba akifanyiwa hivyo anakuwa mtawala lakini imani nyingine wanasema anaongezewa nguvu katika sehemu za kiume kutokana na hayo madawa wanayomfanyia huko porini huku wazazi na mtoto akiwa uchi”alisema mchungaji Faraja Mapunda 
   Ambapo mmoja wa wakazi wa kata hiyo aliyewai kufanyiwa mila potofu ambaye ni Joyce Mtweve alifanyiwa mila hizo akiwa  umri mdogo wa miaka 16 baada ya kupata mtoto wa kwanza wa kiume,anasema alijiskia vibaya kutokana na yale aliyokutana nayo msituni huku akiwa uchi,kwani hata hivyo haoni faida ya kuendeleza mila hizo kwa kuwa hakuna utofauti na watoto wasiopitia mila.
   Viongozi wa serikali hawako mbali katika kuungana na wananchi hao walioungana kupinga mila potofu ambapo Hakim Katabazi ni afisa mtendaji wa kata ya Mavanga,anasema mila potofu katika jamii yake imechangia kwa kiasi kikubwa katika kudidimiza shughuli za uchumi,huku kwa wiki akipokea kesi tatu mpaka nne zinazotokana na mila potofu.













     “Kimsingi lazima tuondokane na hizi mila potofu kwasababu kwa ujumla wake zinachangia kabisa kudidimiza shughuli za kiuchumi,na hata leo nimekutana na  kesi ya mama na baba wamekuja kulalamika kutokana na kesi hizi  lakini,kwa wiki naweza kupokea tatu mpaka nne zinazotokana mambo ya imani potofu,na kesi nyingine wanamalizana wananchi huko huko mitaani”alisema afisa mtendaji.
   Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsele amesema suala la imani potofu katika wilaya hiyo ni kubwa hali ambayo imeendelea kuleta madhara makubwa kuuanana wengine kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.











     “Janga kubwa la hapa Ludewa ni imani potofu ya ushirikina na uchawi, na jambo hili limesababisha watu kutoamini kwamba mtu akiumwa anaweza akatibiwa hospitalini na akifa atakuwa amekufa kwa ugonjwa na baadaye visa vikubwa na kuuana, na jambo hili la ushirikina pia limesababisha kuenea kwa kiwango kikubwa sana kwa maradhi ya ukimwi”alisema Andrea Tsele
    Imeripotiwa na Mwandishi Wetu;Adolf Mwingira

No comments

Powered by Blogger.