Header Ads

Header ADS

Wizara ya maliasili na utalii imepiga marufuku wananchi kuuza nyama pori

      Serikali kupitia Wizara ya maliasili na utalii emetoa agizo la wananchi kutojihusisha na uuzaji wa wanyamapori huku ikiendelea kupitia kanuni na rasimu ambapo imeeleza hadi ifikapo Desemba mwaka 2019,kanuni hizo zitakuwa tayari zimekamilika pia zitawekwa wazi kwa Umma ,maeneo yatakapokuwepo mabucha hayo ,na serikali itaendelea kudhibiti biashara hiyo ,ili mwananchi aweze kununua nyama hiyo kwa njia halali.
    “Haitachukua muda mrefu kanuni hizi zitatoka na tutatoa maelekezo watu wanaotaka kufungua hayo mabucha watayafungua kwa utaratibu gani”.
Hayo yamekuja baada ya Mhe.Rais Magufuli akiwa mkoani Katavi alitoa maagizo kwa Wizara hiyo, huku akikumbushia maagizo ambayo alikwisha yatoa kwamba, ihakikishe inaanzisha mabucha ya kuuza nyama pori ili kuondoa na kudhibiti vitendo vya ujangili na kuwapa fursa wananchi waishi pembezoni mwa hifadhi kupata kitoweo kwa kuwa ni chakula chao cha asili.
















Hayo ameyasema wakati akiwa jijini Arusha na vyombo vya habari Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolfu Mkenda alisema kuwa wizara itaendelea kudhibiti na kuhakikisha hakuna mwananchi hata mmoja atakayeruhusiwa kuuza nyama pori hadi pale serikali itakaporidhia.

“Sasa hivi tunapambana sana na ujangili wawanyama pori ambao wanakamatwa kwa mitego kaskazini mwa Serengeti,imeanza kuingia kidogo maeneo ya seluu,tunakamata watu sana lakini baadhi ya wenyeji wa kule nyama pori ni chakula chao cha asili”Alisema Profesa Mkenda.

Alisema kuwa wanyama wote watakaowindwa kwaajili ya kuuzwa kwenye mabucha lazima wapimwe na waganga/Madaktari kwasababu wanyamapori wanamagonjwa mengi ambayo yamnaweza kuleta athari kwa afya ya binadamu.

“Wanyama pori wana magonjwa kuliko mifugio ya kawaida ni lazima wapimwe,wajulikane wajulikane wale wanaotakiwa kitaalamu kwaajili ya kuliwa ili kuondoa changamoto ya wananchi kupata maradhi yatokanayo na wanyama pori.Alisema Profesa Mkenda.
Agizo hilo limekuja baada ya waandishi wa habari kutaka kujua mchakato wa uanzishaji wa mabucha ya nyama pori utaanza lini na vilevile wizara imejipangaje kuhakikisha zoezi hilo linaepuka ujangili wawanyama.

Profesa Mkenda akijibu maswali hayo amesema kuwa Wizara lazima ipitie Kanuni na rasimu kwani tayari imekamilika vizuri na imeshawasilishwa kwa Waziri,zitajadiliwa,zikishapita zitatolewa rasmi kama kanuni,kisha waanze kufungua mabucha, ili wananchi wanaoishi kando ya hifadhi waweze kupata fursa ya kupata kitoweo hicho kwa bei inayoendana na hali zao kama yalivyo maagizo ya Mhe.Rais.

Ametanabaisha kuwa baada ya kupitishwa na waziri hiyo itakuwa fursa ya kununua nyama pori ndiyo maana hadi sasa wamekuwa wakipeleka maeneo mbalimbali yakiwemo kwenye matamasha ya urithi wetu na wamekuwa wakitoa bure kwasababu hakuna kanuni ya uuuzwaji wa nyama pori.

Alisema wananchi ambao wananishi pembezoni mwa hifadhi ambapo nyama pori ni chakula chao cha asili ,hivyo watahakikisha kuwa kunakuwepo na usawa wa bei ambayo mtu atanunua kwa njia halali,zisijeuzwa mijini mijini peke yake.

Pia alisema kanuni hiyo itatoa mwongozo aina ya wanyama watakaowindwa ,bei na utaratibu mzima wa uwindaji wao na namna ya kufungua mabucha hayo kwa haraka zaidi kwa manufaa ya watanzania kwa ujumla. 
“Mfano mnyama mbogo anatembea na magojwa ambayo yanaweza kumuathiri binadamu ,Yule atakayeruhusiwa kuuza nyama piori lazima apate kibali cha wagani ,hatuwindi wanyama majike,watoto bali wale wqanaokubalika kitaalamu, yanaweza kumwambukiza hatutakuruhu nyama pori kiholela tutakukamata''' .Alisema Profesa Mkenda.
Imeripotiwa na Mwandishi wetu;Adolf Mwingira.

No comments

Powered by Blogger.