Header Ads

Header ADS

Albert Chalamila amesema kuwa wote wanaopinga kuwa serikali haijafanya maendeleo yoyote watachalazwa viboko.

   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kuwa wote wanaosema Serikali hii haijafanya maendeleo yoyote watatandikwa viboko kwasababu watu wengine kujitoa ufahamu kwao ni kawaida.
  Hata hivyo, Ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na wananchi wa Kata ya Utengule- Usangu Wilayani Mbalali baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata hiyo ambacho kinajengwa kwa zaidi ya shilingi milioni 400.
  

  "Wanaopiga maneno maneno huko nje kwamba serikali, kwamba serikali hii hakuna kitu imefanya, kwakweli huwa nawaza kutandika viboko huwa sitanii. Kwasababu haiwezekani kule kuna vitanda vizuri vya kufanyia Operasheni ambavyo vilikuwa vinapatikana Muhimbili leo viko Utengule Usangu alafu unasimama na kitumbo chako unasema hakuna kitu kimefanywa na serikali hii alafu tukuache haiwezekani," alisema RC Chalamila.

"Kwasababu kama huwezi kuona kwa macho aliyokupatia Mungu tutakufahamisha kwa viboko kwamba hapa kuna kitu kimefanyika, kuna wenzetu wachache kujitoa akili kwao ni kawaida."

No comments

Powered by Blogger.