Prof,Ndalichako amesema serikali ipo tayari kupokea Mapendekezo ambayo yatatolewa katika Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema ipo tayari kupokea Mapendekezo ambayo yatatolewa katika Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaoendelea katika Hoteli ya Srena jijini Dar es Salaam.
Hayo ameyasema Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof, Joyce Ndalichako wakati akifungua mkutano wa Sayansi, teknolojia na Ubunifu mkutano huo unaounganisha nchi mbalimbali za kusini mwa Jangwa la Sahara amesema Mkutano huo unalengo la kukutanisha tasisi zinazo fadhiri tafiti za Kisayansi pamoja na kuangalia ni namna gani wanaweza kufanya kazi pamoja.
"Serikali ipo tayari kupokea maoni na mapendekezo ambayo yatatolewa katika Mkutano huo kwa lengo la kuhakikisha tafiti katika nchi yetu na katika nchi za Afrika unaleta tija na chachu ya maendeleo katika nchi za Afrika."
Aidha,Prof ,Ndalichako amesema kuwa ,nchi ya Ujerumaji imetangaza rasmi kufadhili utafiti hapa nchini ili kuongeza chachu ya utafiti na maendeleo ya kisaya na kiteknolojia kwa kuungana na taasisi mbalimbali hapa nchini kwaajili ya kukuza na kuendeleza tafiti za kisayansi ili kuibua vitu vipya zenye kuzalisha katika jamii.
Hata hivyo,amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko tayari kuunga mkono tafiti za kisayansi, kiteknolojia pamoja na ubunifu ili kuwepo na masoko mapya na yenye rasilimali watu wa kutosha katika jamii yetu.
Pia,Prof Ndalichako amewaalika takribani wageni 250 waliopo hapa nchini Kutembelea Vivutio vyote vilivyopo hapa nchini kwani watafurahia pamoja na kuburudisha akili zao.
Aidha,Katika mkutano huo mada zinazoendelea kujadiliwa ni pamoja na kukuza ushirikiano kati ya taasisi ambazo zinafadhili tafiti katika nchi za afrika, kubadilishana uzoefu wa kitafiti katika taasisi zinazofadhili tafiti,kujadiliana mashirikiano mapya ya kufanya tafiti pamoja na miradi mipya ya kitafiti.
No comments
Post a Comment