Header Ads

Header ADS

Chama cha ADC kimetangza kushiriki Uchaguzi wa serikali za mitaa.

   Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimesema licha ya baadhi ya wagombea wake kuenguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, kitashiriki uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 24, 2019.
   Katibu mkuu wa chama cha ADC, Hassan Doyo amezungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya chama hicho na kuweka wazi kuwa hawatajitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019.

 Hata hivyo,wakati chama cha ADC wakieleza kushiriki uchaguzi huo  vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, UPDP, NLD, Chauma, ACT-Wazalendo na CUF vimeshatangaza kutoshiriki uchaguzi huo kwa madai ya kutotendewa haki ikiwa ni pamoja na wagombea wake wengi kuenguliwa.
   “Sisi ni mabingwa wa changamoto hatupelekwi na mihemko ya watu, tunapelekwa na misingi ya chama cha siasa kwa sababu hata walipofuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar wengine walisusa lakini sisi hatukufanya hivyo,” ameeleza Doyo.

No comments

Powered by Blogger.