Header Ads

Header ADS

Wizara ya Kilimo Imekutana na Wakulima na Wadau wakilimo cha Tumbaku Nchini.

       Wizara ya Kilimo imekutana na wadau mbalimbali  na wakulima wa kilimo cha Tumbaku hapa nchini kwa dhumuni la  kujadili changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta  hiyo nakuzitatua hadha ambazo zinawakabili na kuinua sekta ya kilimo cha Tumbaku hapa nchi.
  Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika Jijini Dodoma na kuwakutanisha Wizara ya kilimo, fedha na wadau wa kilimo cha Tumbaku, wakulima na makampuni yanayonunua zao la Tumbaku na wenye viwanda vya Tumbaku, naibu Waziri wa Kilimo Husain Bashe amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kuhakikisha Wanakutana kwa pamoja na kujadili changamoto na vikwazo vyote vinavyopelekea kutoendelea kwa kilimo cha Tumbaku hapa nchini.
"Tumekutana hapa lengo likiwa ni kuangalia ni namna gani tunaweza kutoka hapa tulipo na kwenda mbele, ndio maana tumeshirikisha wadau wote sisi Wizara ya kilimo, fedha, wadau wa kilimo,wenye viwanda na wakulima ili kila mtu ajue nani ni kikwazo na kuanguka kwa sekta hii"
Ameongeza kuwa" zao la Tumbaku uzalishaji wake umekuwa ukishuka siku baada ya siku ukiangalia uzalishaji umeshuka kwa asilimia kubwa toka uzalishaji wa tani laki mojana ishirini (120,000) Hadi kufikia tani arobaini (40) kwa Sasa" Amesema Mhe. Bashe.
Pia ameeleza kuwa,katika kikao hicho wameunda kamati ndogo ambayo itapitia sekta nzima ya kilimo cha Tumbaku na kukutana na wadau wote wa kilimo cha tumbaku na kuja na mapendekezo ya pamoja nini kitanyike na Kodi zipi zipunguzwe kwa Afya ya kilimo cha Tumbaku hapa nchini.
 Hata hivyo,amesema kuwa wameamua kuja na vikao hivyo vya kila kila zao peke yake ili kuona kila zao na tatizo lake kwa matatizo mengi yanatofautiana kwa kila zao na hivyo wameona ni vyema kukaa na wadau wa kila zao kuona namna ya kutatua changamoto za kila  zao.
Aidha,ameongeza kwa kusema kuwa, moja ya changamoto zilizoibuka ni baadhi ya makampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku kutaka kujitoa, na wamejadili na makampuni hayo likiwamo kampuni ya TLTC kutokana na kutorudi kwa VAT return lakini baada ya mazungumzo wamekubali kuendelea na ununuzi wa zao hilo.
 Pia, ameeleza kuwa Lengo kubwa la serikali ni kuona kilimo cha Tumbaku kinaanza kurudi katika uzalishaji wake wa kawaida na kuleta tija kwa serikali na wakulima kunufaika na kazi ambazo wanazifanya.
Aidha,Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme, ambaye ni mdau wa kilimo cha Tumbaku amesema ni muhimu kwa taasisi za Serikali kujenga mazingira mazuri kwa wakulima na wafanya biashara wa zao la Tumbaku ili kuondoa migongano ambayo imekuwa ikitokea Mara kwa Mara.
Mndeme amesema kuwa, kwa pamoja kama wakulima ni lazima  wasimamie ushirikiano katika zao hilo ili iwe rahisi katika hata katika kupanga bei, pia amesisitiza wale wanaopanga ubora wa tumbaku kuwa waaminifu na wazalendo kwa kupanga kwa usahihi.
Naye mmoja wa wakulima ambaye pia ni mwanachama wa chama Cha msingi Tabora, Uyui, Said Shabani, mbali na kumpongeza Naibu Waziri wa Kilimo kwa kuwakutanisha, amesema kwa kikao hicho ameanza kuona mwanga katika sekta ya kilimo na Sasa anaamini uzalishaji utaanza kupanda .

 Naibu waziri wa kilimo akiwa na viongozi na wadau mbalimbali wa kilimo cha tumbaku nchi.

No comments

Powered by Blogger.