Header Ads

Header ADS

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza ratiba ya uchaguzi wa viongozi wake ngazi ya Taifa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza ratiba ya uchaguzi wa viongozi wake ngazi ya Taifa ambapo mchakato huo unaanza na uchukuaji na urejeshaji fomu kuanzia  Novemba 18 hadi Novemba 30, 2019 huku mkutano mkuu ukifanyika Desemba 18, 2019.
     Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vicent Mashinji akizungumza jijini Dar es Salaam amesema kuwa  uchaguzi huo utaanza kwa kuchagua viongozi ngazi ya mabaraza na kufuatiwa na viongozi wakuu wa chama ngazi ya Taifa.

"Tutakuwa na Mkutano Mkuu wa Taifa itakuwa December 18, 2019, tushapeleka mialiko kwa watu mbalimbali, miongoni mwa mambo tutakayoyafanya siku hiyo ni kuchagua Viongozi Wakuu wa Chama.
"Mchakato tunaoanza nao ni kuchukua na kurudisha fomu za Wagombea, huu mchakato unaanza November 18, 2019, wote ambao wangependa kugombea nafasi mbalimbali wanakaribishwa kuja kuchukua fomu, kujaza kwa ufasaha na kwenda kugombea" Amesema  Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji

Amesema baada ya kupitia majina ya wote walioomba, Desemba 8, 2019 kamati tendaji ya baraza la vijana na wazee watakutana na kufuatiwa na mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa mabaraza hayo Desemba 9, 2019.

Ameongeza kuwa Desemba 10, 2019 kamati tendaji ya baraza la wazee na vijana itakutana ambapo ni vikao vinavyofanyika kufuatiwa na mkutano mkuu.

No comments

Powered by Blogger.