Header Ads

Header ADS

Kanisa la Mfalme Zumaridi la fungwa na Serikali.

    Uongozi wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza umepiga marufuku ibada zinazoendeshwa na kiongozi wa kanisa la Mfalme Zumaridi lililoko mtaa wa Iseni kata ya Butimba hadi hapo Serikali itakapojiridhisha kuwa ibada hazikinzani na sheria za nchi.

Kwa mjibu wa agizo la kupiga marufuku hiyo limetolewa  jana Novemba 18, 2019 na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Daktari Philis Nyimbi akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo katika eneo la kanisa hilo.

Amesema kanisa hilo limekuwa likitumia katiba ya kanisa lingine ambalo ni Pentecoste Christian Church of Tanzania  na pia limekuwa likitembea na Katiba ya Kanisa hilo.

DC Nyimbi amesema kiongozi wa Kanisa hilo la Mfalme Zumarid amekuwa akiendesha kanisa hilo bila kufuata sheria za nchi wala maandiko matakatifu kwa kujiita Mungu wa Dunia, Mfalme wakati yeye ni Mwanamke.

No comments

Powered by Blogger.