Header Ads

Header ADS

Katibu Mkuu wa CWT atoa agizo kwa Walimu wa shule za Sekondari Nchini.

     ,Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania Mwalimu Deus Seif  kuelekea kwenye Mitihani ya Kidato cha nne Novemba 04 mwaka huu amewaomba Walimu kote nchini kudumisha uadilifu na kujiepusha na masuala ya udanganyifu katika mitihani hiyo.
    Hayo amezungumza hayo  hii leo Ofisini kwake wakatia akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesma kwa Walimu kazi yao ya kufundisha wameoimaliza na kwa sasa wawaache wanafunzi wafanye mitihani.













    "Katika Mitihani hii ya Kidato cha nne,niwaombe Waalimu wenzangu wote tudumishe uadilifu wetu,tuache haki itendeke maana kosa dogo la Mwalimu linaweza likawagarimu wanafunzi wote"Mwalimu Seif.

"Tuendelee kulinda hadhi yetu ya ualimu kuhakikisha kwamba Mitihani hiyo inafanyika bila udanganyifu wowote,naomba mkirahisishie Chama cha Walimu Tanzania kutokuingia katika doa lolote kuhusiana na mitihani hiyo"Mwalimu Seif.

Katika wakati huo huo Mwalimu Seif ,ametoa salamu za kheri kwa wanafuzni wote nchini wanao tarajiwa kuanza mitihani yao siku ya hapo kesho.

"kwanza niwatakie kila la kheri watoto wetu Mungu awatangulie wakafanye vizuri,lakini pia Walimu wenzangu kazi ya kufundisha mmeimaliza sasa tuwaache watoto wafanye Mitihani".Mwalimu Seif.

No comments

Powered by Blogger.