DC achoma moto Nyavu na vyandarua vya wavuvi haramu wilayani Mwanga.
Thomas Apson ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga ameteketeza kwa moto nyavu aina ya makokoro na vyandarua vya kujikinga na mbu vinavyotumika kwa uvuvi haramu vilivyokamatwa katika oparesheni inayoendelea katika vijiji vinavyolizunguka bwawa hilo vyenye thamani vya shs.39.3mil.
Ambapo amesema kuwa katika oparesheni hiyo wavuvi haramu 14 katika bwawa hilo wametiwa mbaroni kwa kuwatishia polisi wenye silaha waliokuwa doria na kuwataka waweke silaha ili wazichape ngumi kavu kavu.
Kwa upande wake Afisa Tarafa ya Lembeni Bw Gikila Salisali amesema, baadhi ya watumishi wa umma wasiokuwa waaminifu wamekuwa kikwazo katika vita hivyo kwa wanashirikiana na wavuvi haramu na kuiomba serikali iwape boti ili kuimarisha doria ndani ya bwawa.
Lakini pia baadhi ya wananchi waishio katika vijiji hivyo akiwa ni pamoja na bi eda eliakimu na bakari kingazi wakazi wa nyumba ya Mungu wameipongeza serikali kwa kutangaza upya vita hivyo ambavyo wamesema vinaweza kusaidia kupunguza kasi ya uvuvi haramu ambao umekuwa tishio kwa samaki wachanga ambao wangeweza kubadili maisha yao.
No comments
Post a Comment