Header Ads

Header ADS

Waziri Kigwangalla aweka mikakati ya kuvitangaza vivutio vya utalii nchini.

    Dkt,Hamis Kigwangalla ambaye ni Waziri maliasili na utalii  amesema  ataongoza kampeni ya kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika ukanda wa kusini na ukanda wa Kaskazini magharibi kwenye hifadhi mpya za Taifa zilizotangazwa hivi karibuni
   Hata hivyo,  ameeleza kampeni hiyo itawahusisha wasanii na watu maarufu wenye ushawishi katika jamii na inalenga kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivutio vya utalii vilivyo katika hifadhi za Taifa za Ruaha,Mikumi, Nyerere na Burigi – Chato.
     
     Aidha,Dkt.Kigwangalla ameyasema hayo alipokuwa akizugumza na Menejimenti ya Shirika la hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) na wakuu wa Kanda wa shirika hilo jijini Arusha.

     Ameeleza hatua hiyo ya kuwatumia wasanii na watu maarufu wenye ushawishi katika jamii inalenga kuogeza hamasa kwa watanzania wavijue na kuvitembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi hizo hivyo kuongeza idadi ya watalii wa hapa nchini
   .
   Nilipoamua kuutangaza mlima Kilimanjaro na mimi mwenyewe kushiriki kupanda mlima kila mtu alishuhudia nini kilichotokea, kila mtu alikua akiuzungumzia mlima na hii inaongeza umaarufu wa mlima ndani ya nchi huu ni mkakati tunaotakiwa kuutumia katika maeneo mengine” ameeleza Dkt Kigwangalla.

Dkt. Kigwangalla ameiagiza TANAPA iendelee kukusanya takwimu za makundi mbalimbali ya watalii wa ndani wanafanya utalii katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo watazania wanaoshiriki mbio za marathon.

Katika hatua nyingine Waziri wa Maliasili na Utalii ameiagiza TANAPA kuifanyia kazi na kuikamilisha miradi ya ujenzi wa magati na ununuzi wa vivuko na Boti zitakazokuwa zikitumika kusafirisha watalii katika ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi kwenye eneo la Hifadhi ya Taifa ya Saadani.

Amesema gati hizo zitajengwa Dar es salaam, Saadani, Pangani, Pangani na Tanga ili kuwezesha boti hizo kusimama katika maeneo hayo yenye vivutio vya utalii na kushusha watalii wanaotaka kutembelea maeneo hayo.

“Hili ni eneo muhimu sana kwetu na rahisi kuuza huduma zetu za utalii wa ndani ya maji kutokana na uwepo wa visiwa na idadi ya watu wanaokwenda kuvitembelea, Ni lazima tujipange kuzitumia fursa hizi kwa kuwa na boti nzuri zitakazowawezesha watu kufanya utalii, mikutano, harusi na sherehe mbalimbali ndai ya maji na hii itakua ni Biashara kubwa kwetu na njia moja nzuri ya kulitumia vizuri eneo la bahari tulilo nalo” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.
   Aidha ,Waziri Kigwangalla amefafanua kuwa uanzishaji safari za boti za siku kutokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo na kurudi Dar es salaam utawawezesha watalii kwenda kati katika maeneo hayo kwa haraka na ni rahisi kuuza huduma hiyo kwa wageni watakaokuwa wanakwenda kufanya utalii mwisho wa wiki na kuiwezesha Serikali kupata faida ya kiuchumi kutokana na uwepo wa huduma hizo.

No comments

Powered by Blogger.