.Kilimo cha pamba kuanzishwa na Jeshi la Magereza mkoani Simiyu.
Anthony Mtaka ambaye ni mkuu wa mkoa Simiyu amelitaka Jeshi la Magereza kutumia jumla ya Ekali Elfu Tatu na Sabini na Moja zilizopo mkoani hapo kwa kilimo cha pamba ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt.John Magufuli la kutaka jeshi hilo kubadilika na kuingia kwenye mfumo wa uzalishaji ili liweze kuondokana na mfumo wa kutegemea bajeti kuu ya Serikali kulisha wafungwa nchini.
Mkuu wa mkoa huyo ameyaeleza hayo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni mkoani hapo lengo ikiwa ukaguzi wa shughuli za taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo na kuangalia fursa zinazopatikana katika mikoa mbalimbali nchini ili kuweza kulibadilisha jeshi la Magereza hilo
“Mheshimiwa naibu waziri sisi kama mkoa tuko tayari kushikana na jeshi la magereza kwani kuna ardhi ya kutosha na naomba nikuhakikishie hawa wakilima pamba japo ekali mia moja tu na zikauzwa wataweza kufanya mambo mengi ya maendeleo ikiwemo kujenga nyumba za kuishi askari ambazo zitakua ni za kiwango cha juu,” Mtaka alieleza.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa akizungumzalisema Serikali imelipokea jambo hilo kwani ndio lengo hasa la serikali kuona jeshi la magereza linajitegemea katika uendeshaji wake pasipo kutegemea bajeti kuu ya serikali ya Taifa
“Mheshimiwa Rais alishatuagiza tulibadilishe jeshi hili la magereza na tayari tushaanza na tumetenga magereza kumi ya kimkakati nchini ambayo yameteuliwa kuleta mapinduzi katika jeshi, ziara hii ni kuona fursa zilizopo katika mikoa mingine kupitia magereza,nakuahidi jambo hilo tumelichukua kama wizara na muda si mrefu litapatiwa ufumbuzi,” Msauni alieleza.
Hata hivyo,Naibu Waziri Masauni pia alipata nafasi ya kutembelea Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Busega na kuzungumza na mahabusu waliopo kituoni hapo ambapo akuridhishwa na hali ya uchafu katika chumba cha mahabusu kituoni hapo na kuuagiza uongozi kufanya utaratibu wa kusafishwa kwani waliopo ndani ni binadamu na wana haki zao ikiwepo kukaa sehemu safi ili kulinda afya zao.
No comments
Post a Comment