Header Ads

Header ADS

Manchester City imeanza mazungumzo kuhusu mkataba mpya na mshambuliaji wa kimataifa wa England Raheem Sterling, 24. (Mirror)

Mkufunzi wa Leipzig, Julian Nagelsmann na Jose Mourinho wanapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino, aliyefutwa kazi kama mkufunzi wa Tottenham. (Star)
Sterling
Wengine ambao wamejumuishwa katika orodha hiyo ni Eddie Howe wa Bournemouth na Carlo Ancelotti wa Napoli ambao huenda wakapata kazi katika uwanja wa Tottenham Hotspur. (Sun)
Fidia itakayolipwa na Tottenham kwa kumfuta Pochettino na wafanyikazi wake huenda ikafikia £19.6m kiwango ambacho Manchester United ilimlipa Jose Mourinho na timu yake mwezi Disemba 2018. (Mirror)
Pochettino alifutwa kazi kufuatia malumbano kati yake na wachezaji katika chumba cha kubadilisha nguo hali ambayo ilifikia kiwango cha kuathiri utendakazi wake. (Mail)
Pochettino alikataa ombi la Daniel Levy la kumtaka ajiondoe hatua ambayo ilimfanya mwenyekiti wa Spurs chairman kumfuta kazi siku ya Jumanne. (Telegraph)

Red Devils huenda wakalipa hadi £85m kumsaini mshambuliaji wa Salzburg na Norway mzaliwa wa Leeds-Erling Braut Haaland, 19. (Standard)

No comments

Powered by Blogger.