Serikali kuanzisha Masoko ya uhakika ya Asali.
Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii imesema inaendelea na mikakati ili Kuhakikisha kunakuwa na Masoko ya Uhakika ya Asali kwa kuanzisha viwanda katika maeneo mbalimbali Nchini ambapo tayari imetenga bajeti ili Kuanza ujenzi wa viwanda viwili na kukarabati viwanda vingine vitano vilivyopo
Akizindua kamati ya kitaifa ya ushauri wa masuala ya ufugaji nyuki mjini Tabora yenye wajumbe wapatao kumi waziri Kigwangala amebainisha kuwa kuna haja ya kuwa na viwanda vya kuchakata na kufungasha Asali vitakavyosaidia kuwa na Masoko huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na mfumo thabiti wa vyama vya ushirika ili visimamie viwanda hivyo ambapo ametoa muda wa mwezi mmoja Kuhakikisha kuna mifumo ya ushirika.
"Pesa zimetengwa taasisi zipo na zipo tayari kuchangia mizinga zipo tayari kwa ajili ya kujenga hivyo viwanda lakini mfumo haupo mimi nilichokitaka nikuwepo na mfumo thabiti wa ushirika kwani ndiyo msingi wa kufanikiwa kwenye utekelezaji wa mpango huu"Amesema Kigwangala
Katika hatua nyingine Waziri Kigwangala amekabidhi Mizinga miasita kwa kikundi chat ufugaji nyuki IPOLE na mizinga miatano katika chuo cha ufugaji nyuki Tabora huku akiziagiza taasisi zilizo chini ya wizara yake zikuwemo TANAPA, TAWA na TFS kutengeneza mizinga elfusita Kila taasisi ili zigawiwe katika vyama vya ushirika vitakavyoanzishwa
Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Ezekiel Mwakalukwa Amesema takwimu zilizopo za mizinga katika kikundi cha Ipole ni takribani elfu kumi na mbili ya magome ya miti na mizinga ya maboxisi ni mizinga miamoja licha ya kuwepo na juhudi kubwa ya ufugaji nyuki lakini kwa sehemu kubwa inaharibu Mazingira
Aidha pamoja na kukabidhi mizinga Huyo waziri wa maliasili na utalii pia ameiomba bodi kumshauri kuhusu ujenzi wa viwanda na muundo mzuri ambao utafaa katika kuvisimamia na namna ya upatikanaji wa Masoko ya Uhakika.
No comments
Post a Comment