Maonesho ya wiki ya kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa yazinduliwa na waziri Jafo.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo leo amezindua maonesho ya wiki ya kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa (NCD) yanayoendelea katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Kabla ya uzinduzi huo Waziri Jafo alitembelea baadhi ya vibanda kuona huduma mbalimbali zinazotolewa ambapo ameridhishwa na huduma hizo ambazo zimeonekana kuwavutia wakazi wengi wa jiji la Dodoma.
Aidha, Waziri Jafo amehimiza wananchi kuwa na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kubaini magonjwa mapema na kuweza kupata matibabu na ushauri kutoka kwa madaktari ikiwemo kuwa tabia ya kufanya mazoezi mara dufu.
Hata hivyo, Waziri huyo ameishukuru Wizara ya afya kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI katika maandalizi ya maonesho hayo ambapo amewataka wananchi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi ili wapime afya zao na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu. Maonesho hayo yanaendelea kwa wiki moja mpaka tarehe 14 Novemba 2019.

No comments
Post a Comment