Mbarawa ameagiza waliotumia Fedha za mradi wa Maji wakamatwe.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, - John Mwaipopo kuwakamata Viongozi wa Jumuiya za Watumiaji Maji wa Nkinga na Matinje, kwa tuhuma za kula fedha zilizotokana na malipo ya watumiaji maji.
Mbarawa ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake wilayani Igunga, ambapo amepokea malalamiko ya Wakazi wa wilaya hiyo kuhusu matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maji.
Pia amesisitiza kuwa, Viongozi wote wa Jumuiya hizo za Watumiaji maji wanaotuhumiwa kula fedha hizo ni lazima wakamatwe na wazirudishe fedha hizo ili ziweze kusaidia kuboresha miradi hiyo ya maji.
Aidha, Mbarawa, amesema kuwa ni kosa kwa Viongozi wa Jumuiya za Watumiaji Maji nchini kukusanya fedha zinazotokana na mauzo ya maji bila kuziweka Benki, kwa kuwa vitendo vya aina hiyo ndivyo vimechangia miradi mingi ya maji kufa kutokana na kukosa fedha pindi inapotakiwa kufanyiwa ukarabati.

Hata hivyo,Katika hatua nyingine Waziri Mbarawa amesema kuwa, Serikali itahakikisha inapeleka maji ya kutoka Ziwa Viktoria katika eneo la Nkinga, ili kupunguza tatizo la maji katika eneo hilo ambalo lina Hospitali ya Rufaa ya Nkinga ambayo inategemewa na Wananchi wa Kanda hiyo.
No comments
Post a Comment