Mbunge aishukuru Serikali kwa kusaidia kuweka Lami
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kuwasaidia kuweka lami baadhi ya barabara zilizopo kwenye Jimbo.
Pia Mbunge huyo amewataka Wananchi kumpa ushirikiano Mkandarasi ambaye anatekeleza ujenzi huo ili aweze kutekeleza kazi yake kwa wakati kutokana na kwamba amepewa muda wa miezi saba.
Pia Mbunge huyo amewataka Wananchi kumpa ushirikiano Mkandarasi ambaye anatekeleza ujenzi huo ili aweze kutekeleza kazi yake kwa wakati kutokana na kwamba amepewa muda wa miezi saba.
Balozi Adadi aliyasema hayo wakati wa halfa ya utiaji wa saini kati ya kati ya Halmashauri ya Muheza na Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya SIMAC Limited kutoka Dar kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za mita 800 kwenye mji huo.
Alisema kwamba utiliaji saini huo umeonyesha namna serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha inaboresha miundombinu kwenye miji mbalimbali hapa nchini.
Mbunge huyo alisema kwamba barabara ni kilomita ya pili ambayo itaanzia Kilimanjaro Bar, Darajani, relini mpaka hospitali ya Teule Muheza na baadae kufika mpaka kwenye kipande ambacho kinatumika na wananchi kwenye maeneo ya karibu na soko la Muheza.
“Serikali ya awamu ya tano imeweza kutusaidia kuweka lami ni jambo kubwa na la faraja kubwa kwetu hivyo kwa sababu lami itawekwa kwenye mji wetu hakikisheni mnapa ushirikiano na niwaombe msimpe vikwazo vya namna yoyote ile “Alisema Balozi Adadi.
Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo Meneja wa Tarura wilaya ya Muheza Mhandisi Joseph Kahoza alisema kwamba mkandarsi aliyekabidhi mkataba huo ni wa barabara za mita 800 kwa ajili ya kuweka lami kwa mji wa muheza.
Alisema mkandarasi huyo ataanza kufanya kazi hiyo kuanzia barabara ya Kilimanjaro darajani, relini mpaka teule ambao utakuwa na thamani ya milioni 386 huku akieleza barabara nyengine ya mita 200 zinazokarabatiwa mjini humo zitatumia zaidi ya milioni 60..
Naye kwa upande wake Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi SIMAC LTD kutoka Dar Felix Chawe ambao wamekabidhiwa barabara hiyo alisema kwamba anajisikia furaha kupata nafasi ya ujenzi huo huku akihitaji ushirikiano na kuhaidia kufanya kazi kwa uwezo wake wote na maelekezo yaliyopo kwenye mkataba.
No comments
Post a Comment