Header Ads

Header ADS

Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kufika Mkoani Morogoro kushughulikia vitambulisho vya Taifa

  Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kufika Mkoani Morogoro leo na ikiwezekana akae Mkoani humo hata siku tatu ili kushughulikia tatizo la Watu wengi kukosa vitambulisho vya Taifa huku Mkoa mzima ukiwa na Ofisi moja pekee ya NIDA.
       
  Aidha Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo akiongea na wananchi wa Msamvu, Morogoro akiwa njiani akielekea mkoani Dodoma
  “Nimemtaka Mkurugenzi Mkuu NIDA afike hapa Morogoro ashughulikie hii changamoto ya vitambulisho na nataka huduma hii iende kila Wilaya, haiwezekani Watu wasafiri kutoka Wilayani kuja Mjini au muwape nauli na hela ya Gesti,na hili litazamwe Nchi nzima Watu wapewe vitambulisho” amesema.
  Ameongeza  kwa kusema kuwa, "Watu wanataka kusajili laini zao za simu na mambo mengine lakini zoezi la vitambulisho linacheleweshwa na Watu wachache, suala la NIDA linaenda polepole sana, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA nitahitaji unipe na tathmini ya zoezi lote Nchi nzima".

No comments

Powered by Blogger.