Header Ads

Header ADS

Mwanamke Mmoja Mkoani Njombe anashikiliwa na polisi kwa kosa na kumchinja Mwanae na Kumla Nyama.

    Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Christina Mlelwa mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Kijiji cha Mavanga  wilayani Ludewa mkoa wa Njombe anashikilikiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumchinja mwanae Joseph Gumbilo(4) mwenye ulemavu wa viungo na kumla nyama.



Awali akizungumzia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrew Tsere amesema mapema baada ya kupokea taarifa za tukio hilo alilazimika kufika eneo la tukio na kumhoji mtuhumiwa ambaye alikiri kutekeleza mauaji ya mwanae na kisha kumkata viungo vyake  na kumla huku viungo vingine kuvitupa porini na chooni.
Hata hivyo,tukio hilo limeleta mshituko kwa kamati ya ulinzi na usalama mkoa na lilimstajabisha  mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka na kufika katika kijiji hicho kuzungumza na wananchi na kisha kutoa agizo kwa wakuu wote wa  wilaya za mkoa huo kukamata kijiji kizima na kuweka lockup endapo watagoma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu matukio ya mauaji.
Pia,katika hatua nyingine Olesendeka ameliagiza jeshi la polisi kusaka ukweli wa tukio hilo haraka na wahusika kufikishwa mahakamani kama ambavyo katiba inalinda haki ya kuishi ya kila binadamu bila kujali ulemavu wake.
Hata hivyo,  Jeshi la polisi,  lilifanya mahojiano ya awali na mama huyo ambaye anaonekana kuwa na matatizo ya akili amekiri kuua na kukata vipande vipande na kumla nyama huku masalia mengine ikiwemo fuvu la kichwa na miguu akiyatupa porini hatua ambayo ililazimu kamati ya ulinzi kuvamia pori na kukuta vitu hivyo.
Aidha  Mume wa mama huyo  bwana Daniel Gumbilo amesema mke wake alishawahi kufanya jaribio kama hilo miaka ya nyuma kwa mototo wao mwingine anayesoma ambapo majirani walinusuru maisha ya mtoto wao .
Pia,Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema jeshi linaendelea kuchunguza kwa kina zaidi kuhusiana na tukio hilo ili wahusika wapewe haki yao ya hukumu ya uovu wao.
Kwa upande wa mtendaji wa kijiji cha Mavanga Fadhiri Tajiri amesema ni kweli tukio hilo limetokea na kwamba taarifa zaidi anasubiri muongozo kutoka kwa viongozi wake.
"Ni kweli Hilo tukio lipo lakini viongozi wangu wamesema wapo njiani wanakuja nasubiri muongozo wa kutoka kwao"alisema Tajiri.

No comments

Powered by Blogger.