Watafiti nchini wameombwa kuisaidia jamii kwa kuja na teknolojia mpya ya mbegu kwa upande wa chakula ya muda mfupi.
Watafiti nchini wameombwa kuisaidia jamii kwa kuja na teknolojia mpya ya mbegu kwa upande wa chakula ya muda mfupi na isiyo hitaji maji mengi ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi.
Hayo, yameelezwa na Mkurugenzi mkuu wa Jukwaa la Wadau wa Kilimo Audax Rukonge wakati kizungumza na waandishi wa wahabari kuhusiana na Mkutano wa mwaka ambao unatarajia kufanyika wiki ijayo lengo likiwa ni kuangalia changamoto na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia ya nchi na fursa zipi zinapatikana kwenye mabadiliko hayo.
Rukonge alisema ipo haja kwa watafiti kuleta teknolojia mpya ya mbegu zitakazoendana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi ili wakulima kuweza kunufaika wakati wote hali ya hewa itakavyokuwa.
“Mabadiliko ya Tabia ya nchi haya tabiriki kuna wakati inaweza kuwa jua sana au mvua kubwa lakini hali zote hizo wakulima wanahitaji kuendelea na kilimo hivyo watafiti wetu wanaweza kuja na teknolojia ya mbegu mbadala itakayoweza kuhimili vipindi vyote vya hali ya hewa”,alisema Rukonge.
Hata hivyo, aliongeza kwa kusema kuwa kunahitajika teknolojia itayowezesha wakulima kuhifadhi chakula vizuri ikiwa uzalishaji ulikuwa ni wakasi zaidi.
“Hata kama tumezalisha chakula kingi kuliko uwezo wetu wa maghala ya kutunza ,Watafiti wetu pia wanatakiwa kuja nawaje na teknolojia nyepesi,rahisi na rafiki kwa makundi mbalimbali kwa jamii kuhakikisha kwamba mazao haya ambayo yamezalishwa kwa wingi hayapotei kwasababu tu hatuna teknolojia nzuri”,aliongeza Rukonge.
Pia, Mkutano huo ujadili fursa mbalimbali zilizopo katika mabadiliko ya Tabia ya nchi ambapo fursa zenyewe ni kama uvunaji wa maji,kuwekeza kwenye Teknolojia ya Uzalishaji wa mbegu na Teknolojia ya Utunzaji wa Mazao.
Hata hivyo,Mkutano huo ni wa siku mbili unatarajia kufanyika Jijini Dodoma wiki ijayo.
No comments
Post a Comment