Header Ads

Header ADS

Serikali yaamasisha matumizi ya Gesi ili kupunguza uharibifu mazingira.

       Dk Medard Kalemani  ambae ni Waziri wa Nishati ameeleza kuwa  serikali imeendelea kusisitiza katika matumizi ya gesi kwa wananchi ili kupunguza uharibifu wa mazingira ndani ya nchi.
  Amesema hayo leo  alipokuwa akizungumza na washiriki kutoka Taasisi mbalimbali nchini katika mkutano wa majadiliano ya Wiki ya Azaki inayoendelea jijini Dodoma.
   Dk Kalemani amesema kuwa wananchi kwa sasa wameanza kujenga  mazoea ya kutumia gesi lengo ni kupunguza ukataji wa miti hovyo ambayo inachangia kuharibu mazingira.
Amesema sekta ya uziduaji ni  muhimu sana ambayo inapaswa kutunza ili iweze kuleta manufaa katika nchini jambo ambalo linahitaji kuangaliwa.kwa.kiasi.kikubwa.
    Aidha,Waziri wa nishati  amesema kuwa kwa sasa tunahitaji kutumia gesi kwa kuhakikisha rasimali hizo zinatumika ipasavyo.
  Dkt.Kalemani amesema kuwa Tanzania inarasimali kubwa ya gesi lakini bado hatujagundua Mafuta,ila jitihada za serikali kutafuta zinaendelea.
   Amesema kuwa  kwa upande wa gesi toka trion mbili trion 57.5 jambo linalopaswa kuipongeza serikali ya awamu ya tano,hivyo Trion 57.5 zinapaswa kupongezwa kutokana na ongezeko hilo.















     Akizungumzia kuhusiana na suala Mafuta amesema kuwa serikali inaendelea na jitihada za utafutaji Mafuta.
   Aidha waziri Kalemani amewataka AZAKI kutoa taarifa sahihi na zitoke kwa wakati ili wananchi waweze kujua nini kinaendelea ikiwemo kupata takwimu sahihi.
    Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Madini Stanislaus Nyongo,amesema kuwa Serikali imejipanga kuanza kusafisha dhahabu hapa nchini ili kuongeza thamani yake hali iatayosaidia kuongeza pato la taifa na kuhifadhi fedha Benki kuu kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya baadae.
    Aidha amesema kuwa watajenga  kituo cha kuchakata dhahabu jijini Dodoma na mkoani Geita vyote vitatumika kwa ajili ya kusafisha dhahabu lengo likiwa ni kuongeza thamani ikiwemo pato la taifa litokanalo na dhahabu.
    Mhe.Nyongo amesema kuwa dhahabu inayopatikana hivi sasa ni asilimia 80 wanahitaji isafishwe hapa nchini na.kufikia asilimia 99.9 ili BOT iweze kupata fedha kutokana na dhahabu hiyo.
   Lakini pia, Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Rasirimali Rachel Chagonja amesema kuwa jukwaa la uzinduaji lina lengo la kuendeleza mijadala katika sekta ya madini,Mafuta na gesi asilia hapa nchini kwa lengo la kupambana taarifa na uelewa wa sekta ya uziduaji.
    “Jukwaa hilo linasaidia jamii kufahamu vipaumbele na fungamanisho la mikakati iliyopo kwenye kusimamia sekta ya jukwaa la uziduaji”amesema Chagonja

No comments

Powered by Blogger.