Header Ads

Header ADS

CHADEMA,mkoa wa Njombe wametangaza kususia shughuli zote za maendeleo

     Katika Mkoa wa Njombe Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimetangaza kutoshiriki shughuli zote za kimaendeleo  katika maeneo ambayo kwa mujibu wao viongozi wake watapitishwa kwa ubabe na chama cha mapinduzi.
   Ambapo akizungumza katika mahojiano na radio kings iliyopo mjini Njombe mkoani humo katibu wa Chadema mkoa wa Njombe Alatanga Nyagawa,amesema anashangazwa na mchezo unaofanywa na chama cha mapinduzi kwa wagombea wao wakati wa urejeshaji wa fomu hivyo ni lazima wasusie shughuli za maendeleo kabla ya kwenda kudai haki sehemu nyingine mara baada ya kulazimisha viongozi kupita bila kupingwa.
     “Kwa kweli kilichobaki sasa ni kuwaambia wanachama wetu kususia hawa viongozi watakaopitishwa kwa ubabe, ni lazima tususie,tutakwenda kudai haki popote pale lakini kwanza tunasusia kwasababu huyo mwenyekiti anakuwa ameteuliwa tayari,lazima tutangaze kwa wananchi kwamba tunasusia shughuli za maendeleo katika maeneo yote ambayo watalazimisha watu wao wapite bila kupingwa”alisema Alatanga Nyagawa.

   











     Aidha,Nyagawa amesema anashangazwa kuona baadhi ya maeneo ikiwemo mjini Makambako mgombea wao kuenguliwa kwasababu ya kutokuwepo kwa namba moja katika kadi yake kwa kusahau kuiandika katika fomu.
   Venas Msungu ni miongoni mwa wasimamizi wa uchaguzi mkoani Njombe anayesimamia halmashauri ya mji wa Njombe,amesema fomu ya wagombea ni kama mtihani hivyo ni lazima ichukuliwe kwa uzito hivyo baadhi ya wanasiasa wamekosa weledi na kutekeleza tofauti na maelekezo.
   “Wanasiasa wengi weledi au elimu ya siasa haijakomaa vya kutosha,unaambiwa ufanye hivi wewe unatekeleza vitu tofauti kwa hiyo kazi ya msimamizi sio kurekebisha fomu ya mgombea,mgombea inatakiwa atambue kinachotakiwa kwenye fomu na aweze kutekeleza”alisema  Venas Msungu msimazi wa uchaguzi Njombe mjini
    “Halmashauri ya mji wa Njombe fomu zilizochukuliwa,CCM walichukuwa fomu 1030 CHADEMA 341 na ACT fomu 1 kwa hiyo wakati mwingine mtu anapolalamika ni vizuri mkatumia takwimu anaweza akaja mtu akalikuza tatizo likawa kubwa sana,muulize alipeleka wagombea wangapi?”aliongeza Venas Msungu msimamizi wa uchaguzi
   Lakini pia, Selemani Jafo ambae ni waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa tamisemi amesema serikali haitaweza kupoteza haki ya mtu pindi itakapobainika ameonewa.
 

No comments

Powered by Blogger.