Header Ads

Header ADS

TCRA.Yatoa mafunzo

Mpango wa kuweka mabango ya anwani za makazi na postikodi usifanywe kisiasa bali ufuate taratibu na sheria zilizowekwa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi na postikodi kwa watendaji  mamlaka za serikali za mitaa Manispaa za Mkoa wa Singida  ambayo yameandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

”Suala ili naomba lisifanywe kisiasa lifuate sheria na taratibu zilizopo kwani katika maeneo mengine lilichelewa kufanyika kutokana na wanasiasa kutaka majina yao yawekwe kwenye vibao vya mitaa” alisema Nchimbi.

Alisema mpango huu wa kitaifa ni muhimu sana kwani unasaidia wakati wa matukio ya dharura kama moto na kuwafuata wagonjwa katika maeneo yao yanayojulikana tofauti na ilivyo hivi sasa.

Nchimbi alitaja faida nyingine kuwa utaweka vizuri mipango miji katika maeneo wanayoishi wananchi na utapunguza migogoro ya ardhi na utambuzi wa watu wanapoishi na kupata huduma
za kijamii kwa urahisi.

chimbi alitumia nafasi hiyo kuwaomba wataalamu wa mkoa wa Singida ambao wamepata mafunzo hayo kwenda kufanya kazi hiyo kwa bidii na weledi huku wakiweka maslahi ya Taifa mbele.

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Antonio Manyanda alisema TCRA imekuwa ikitekeleza majukumu yake katika mradi huo kama ilivyoelekezwa katika sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003 ambayo inalenga kuboresha maisha ya watanzania kwa kupambana na umaskini.

Alisema mpango huo ulianza katika jiji la Arusha ambapo baadhi ya kata ziliwekewa miundombinu ya anwani kama sehemu ya mfano (pilot) na baada ya hapo uliendelea katika jiji la Dodoma ambapo ushahidi wa miundombinu unaonekana.


No comments

Powered by Blogger.