Wabunge wa Tanzania waanza kutumia Tablet
Wabunge nchini Tanzania wataanza kutumia tablet kwa ajili ya kazi za bunge, huku bunge hilo likiondokana na matumizi ya karatasi.
Wabunge walikabidhiwa vifaa hivyo Jumatatu kabla ya kuanza kwa vikao leo Jumanne mchana katika mji mkuu wa nchi hiyo Dodoma.
Katika akaunti ya rasmi ya Twitter ya bunge zilitumwa picha za wabunge wakipokea Tablet na ujumbe uliosema wanalenga kuachana na matumizi ya karatasi :
Wabunge walikabidhiwa vifaa hivyo Jumatatu kabla ya kuanza kwa vikao leo Jumanne mchana katika mji mkuu wa nchi hiyo Dodoma.
Katika akaunti ya rasmi ya Twitter ya bunge zilitumwa picha za wabunge wakipokea Tablet na ujumbe uliosema wanalenga kuachana na matumizi ya karatasi :
Waheshimiwa Wabunge wapatiwa tablets kwa ajili ya kuwasaidia katika matumizi ya shughuli za Bunge lengo likiwa ni kuondoa matumizi ya karatasi. Zoezi hilo limefayika siku moja kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kumi na Saba wa Bunge Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge Stephen Kigaigai alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuhifadhi pesa ambazo serikali imekuwa ikizitumia kuchapisha na kunakili nyaraka za serikali.
" Hata hivyo tumeziomba wizara husika kuja na baadhi ya nyaraka kwa ajili ya kuweka rekodi yake. Kwa mfano kwa matumizi katika maktaba," alisema.
Bwana Kigaigai anasema imekuwa ikichapisha nakala 500 za nyaraka za kutumiwa katika shughuli za bunge kwa siku lakini kwa sasa zitakuwa chini ya nakala 10.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wabunge wote leo wameingia bungeni na Tablet.
Spika wa bunge hilo Job Ndugai amezitaka taasisi nyingine nchini Tanzania kuiga mfano wa bunge kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kupunguza matumizi ya karatasi.
Anatarajia hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama ya kuchapisha kutoka shilingi bilioni 1.2 sawa na $519,000 hadi shilingi milioni 200.
Bunge limenunua takriban tableti 450 zenye thamani ya shilingi milioni 900 sawa na $389,000.
No comments
Post a Comment