Waziri Selemani Jafo,ametoa agizo kwa wagombea walioenguliwa.
Selemani Jafo,ambae ni Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amezitaka kamati za rufaa kusikiliza vyema kero za watu wenye malalamiko, ikiweno za wagombea waliokatwa majina yao na kuhakikisha wanayarejesha ili na wao waweze kupata haki zao za msingi.
Hayo ameeleza leo Novemba 5, 2019, wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma na kuwataka wale wote wenye malalamiko na mapingamizi ya zoezi la uchaguzi linaloendelea, kufika katika ofisi husika ili kuepusha migongano ya kimaslahi.
“Kulalamika ni jambo la msingi na kuna nafasi nzuri ikiwemo nafasi ya mapingamizi na kukata rufaa na ndio maana nimewaambia watu wetu wote wa zile kamati za rufaa, zisikilize malalamiko ya watu kwa msingi na hoja na kuyafafanua vizuri, wale wote ambao watakuwa wameonewa na majina yao yametolewa, lazima warejeshwe na wapate haki yao kama kushindwa waende kushindwa huko” amesema Waziri Jafo.
Lakini pia,Waziri Jafo amekemea baadhi ya watendaji wa Serikali za Mitaa, kukataa kusikiliza malalamiko na kuwataka kuacha mara moja tabia hizo na kwamba wanapaswa kusikiliza malalamiko yote yaliyondani ya uwezo wao na kama watashindwa wayapeleke ngazi za juu.
No comments
Post a Comment