Header Ads

Header ADS

Watendaji wa mamlaka za Serikali za mitaa Singida, wapewa mafunzo yautekelezaji wa mfumo wa Anwani za makazi na postikodi.

     Mpango wa kuweka mabango ya anwani za makazi na postikodi usifanywe kisiasa bali ufuate taratibu na sheria zilizowekwa.
    Ambapo Dkt. Rehema Nchimbi Mkuu wa Mkoa wa Singida ametoa wito huo ambapo alikuwa mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi na postikodi kwa watendaji  mamlaka za serikali za mitaa Manispaa za Mkoa wa Singida leo ambayo yameandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
   ” Suala ili naomba lisifanywe kisiasa lifuate sheria na taratibu zilizopo kwani katika maeneo mengine lilichelewa kufanyika kutokana na wanasiasa kutaka majina yao yawekwe kwenye vibao vya mitaa” alisema Nchimbi.
    Aidha alieleza kuwa mpango huu wa kitaifa ni muhimu sana kwani unasaidia wakati wa matukio ya dharura kama moto na kuwafuata wagonjwa katika maeneo yao yanayojulikana tofauti na ilivyo hivi sasa.
  Nchimbi alitaja faida nyingine kuwa utaweka vizuri mipango miji katika maeneo wanayoishi wananchi na utapunguza migogoro ya ardhi na utambuzi wa watu wanapoishi na kupata huduma
za kijamii kwa urahisi.















     Lakini pia, Nchimbi alitumia nafasi hiyo kuwaomba wataalamu wa mkoa wa Singida ambao wamepata mafunzo hayo kwenda kufanya kazi hiyo kwa bidii na weledi huku wakiweka maslahi ya Taifa mbele.
   Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Antonio Manyanda alisema TCRA imekuwa ikitekeleza majukumu yake katika mradi huo kama ilivyoelekezwa katika sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003 ambayo inalenga kuboresha maisha ya watanzania kwa kupambana na umaskini.
    Aidha,alieleza kuwa mpango huo ulianza katika jiji la Arusha ambapo baadhi ya kata ziliwekewa miundombinu ya anwani kama sehemu ya mfano (pilot) na baada ya hapo uliendelea katika jiji la Dodoma ambapo ushahidi wa miundombinu unaonekana.

No comments

Powered by Blogger.