Wanajeshi 49 Wauawa Kaskazini Mwa Mali
Wanamgambo wa kaskazini mashariki mwa Mali wamewaua wanajeshi 49 katika shambulio lililotokea jeshini, mkuu wa jeshi ameandika katika kurasa zake za Facebook.Shambulio hilo linatajwa kuwa hatari zaidi ya iliyowahi kutokea miongo iliyopita.
Katika kurasa ya twitter, jeshi limeelezea kuwa shambulio hilo ni la kigaidi.Mali imekuwa ikikabiliana na vurugu za mara kwa mara tangu mwaka 2012, wakati ambao wanamgambo wa kiislamu waliposhambulia kaskazini mwa nchi hiyo.
Shambulio hilo linatajwa kuwa hatari zaidi ya iliyowahi kutokea miongo iliyopita Katika kurasa ya twitter, jeshi limeelezea kuwa shambulio hilo ni la kigaidi Mali imekuwa ikikabiliana na vurugu za mara kwa mara tangu mwaka 2012, wakati ambao wanamgambo wa kiislamu waliposhambulia kaskazini mwa nchi hiyo.
Kwa msaada wa Ufaransa, jeshi la Mali lilikuwa linalinda usalama wa eneo hilo lakini bado vurugu zinaendelea.Vurugu hizo imeenea hata katika mataifa mengine ya jirani.Awali iliripotiwa kuwa askari 54 waliuawa, taarifa aliyoitoa msemaji wa serikali Yaya Sangare.
Hakuna kikosi cha kigaidi ambacho kimekiri kuhusika na shambulio hilo katika maeneo ya Indelimane huko Menaka.
Askari 38 waliuawa wakati ambapo kambi mbili za jeshi zilipovamiwa karibu na mpaka wa Burkina Faso mwishoni mwa mwezi septemba .
Mali pamoja na Burkina Faso, Chad, Niger na Mauritania - ni miongoni mwa nchi ambazo majeshi yao yanafadhiliwa na Ufaransa.
Vikosi vitano vya taifa vinashuku kuwa wajumbe wa Ansarul walishambulia mwezi septemba.
Kundi la Ansarul Islam, likimaanisha kuwa watetezi wa dini ya kiislamu, lilianzishwa mwaka 2016 na mhubiri maarufu Ibrahim Malam Dicko.
Mwaka 2012, iliripotiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu Kaskazini Mwa Mali Walishambulia Maeneo hayo.
No comments
Post a Comment