Header Ads

Header ADS

Watahiniwa wanne washindwa kufanya mitihani kwa Ujauzito

Takribani watahiniwa elfu 1319 Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi  wamefanikiwa kufanya  mtihani wa kidato cha nne  690 wakiwa ni wavulana na 629 wakiwa ni wasichana kati ya shule 13 zilizopo ndani ya manispaa.
    Akitoa takwimu hizo Afisa Elimu sekondari manispaa ya mpanda Enelia John  amesema watahiniwa wanne ndio hawajafanya mtihani kwa kubainika kuwa na ujauzito.
  
Akizungumza na Machweo Communication News .amesema  wazazi ndio chanzo kikubwa cha kuwatengenezea watoto mazingira ya tabia hatarishi kwa kuwatelekeza kwa muda murefu kwa kisingizio cha kubanwa na shughuli za kilimo hivyo watoto hukosa malezi ya mzazi na kujiingiza kwenye tabia zinazohatarisha ndoto zake.

"Mzazi anaondoka kwenda shambani na anaweza akamaliza miezi 3 hayupo nyumbani halafu familia anamuachia binti au kijana ambae bado anasoma mtoto  hana uwezo wa kujiongoza atafanya kitu anachoona kinafaa kwa muda huo mwisho wake ataanza kuvuta bangi na wengine kuanza  mahusiano mwisho wake mimba".

Aidha amewataka wasimamizi wa mitihani kuhakikisha wanasimamia vizuri kama walivyopewa mafunzo ili kuhakikisha wanafaulisha Mwanafunzi wenye uweledi na watakayoijenga Tanzania ya kesho na mpaka sasa hakuna mtihani uliovuja.

No comments

Powered by Blogger.