Conservative chanyakua viti vya Leba katika ushindi mkubwa
Kiongozi wa chama cha Conservative Boris Johnson amewashukuru wapiga kura wa Uingereza kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa Disemba.
Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya chama chake kushinda zaidi ya viti 326, Boris Jonhson amesema kwamba hatua hiyo inaipatia serikali mpya fursa ya kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia ya raia wa Uingereza ili kuliimarisha taifa hilo.
Chama cha Boris Johsnon kilihitaji kujipatia viti 326 ili kutangazwa kuwa mshindi lakini kufikia sasa kimepitisha idadi hiyo na kufikia viti 334.
Waziri huyo mkuu amesema kwamba uamuzi huo unampatia jukumu la kufanikisha Brexit na kuiondoa Uingereza katika muungano wa Ulaya
Hatua hiyo inajiri muda mchache baada ya mpinzani mkuu wa Boris Jonson Jeremy Corbyn kusalimu amri na kusema kwamba hatokiongoza tena chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Uamuzi huo wa kiongozi wa Leba unajiri huku chama hicho kikikabiliwa na matokeo mabaya zaidi ya uchaguzi katika miongo kadhaa.
Chama cha Conservative kimeshinda baadhi ya viti katika ngome za chama cha Leba.
Chama cha Leba kimepoteza viti kaskazini mwa England , Midlands na Wales yakiwa ni maeneo yaliopiga kura ya Brexit katika kura ya maoni ya 2016.
Leba inatarajiwa kushinda viti 61 ikiwa ni chini ya viti ilivyoshinda 2017 imedaiwa.
Baadhi ya maeneo bunge kama vile Darlington ama Workington , kaskazini mwa England yataongozwa na mbunge wa Chama cha Conservative kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa- ama katika matukio ya Bishop Auckland na Blyth Vally kwa mara ya kwanza tangu viti hivyo kubuniwa.
Lakini Leba kimeshinda kiti cha eneo bunge la Putney, kusini magharibi mwa London kutoka kwa Conservative.
Chama cha Uskochi cha kitaifa kimepata ushindi wake wa kwanza usiku wa kura , kikishinda eneo bunge la Rutherglen na Hamilton magharibi kutoka kwa chama cha Leba na Angus kutoka kwa Conservative.
Matokeo hayo ambayo yanatoka katika vituo 144 vya kupigia kura yameimarishwa ili kuangazia matokeo rasmi.
Imebainika kwamba Conservative watapata wabunge 357 ikiwa ni wabunge 39 zaidi ya uchaguzi wa 2017 kura zote zitakapohesabiwa.
Chama cha Leba kitajipatia wabunge 201, SNP wabunge 55 , LIberal Democrats 13, Plaid Cymru 4 The Greens 1 brexit Party 0.
Huku matokeo ya maeneo bunge 175 yakiwa yametangazwa , ongezeko la wastani katika kura ya chama cha Conservative ni asilimia 2 ikiwa ni pointi moja ya kilichotarajiwa katika kura hiyo.
Kura ya chama cha Leba ilipungua kwa asilimia 9 kulingana na utabiri wa matokeo ya kura hiyo yasio rasmi.
Nchini Uskochi, kumekuwa na ongezeko la asilimia 9 katika chama cha kitaifa cha Uskochi - ikiwa ni kiwango cha chini ya ilivyotabiriwa kwa asilimia 13 lakini SNP kinaelekea kushinda viti 55.
Waziri wa maswala ya ndani wa chama cha Conservative Priti Patel alisema kwamba serikali itahakikisha kwamba Brexit inafanyika kwa haraka kabla ya Christmas kupitia kuwasilisha miswada iwapo serikali yake itarudi mamlakani.
No comments
Post a Comment