Mbowe atetea tena kiti cha Uenyekiti CHADEMA
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amechaguliwa tena katika nafasi hiyo baada ya kupata kura 886 sawa na 93.5% dhidi ya mpinzani wake Cecil Mwambe aliyepata kura 59 sawa na 6.2%. Mbowe atatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.
Matokeo hayo yametangazwa leo Alhamisi Desemba 19, 2019 saa 11 alfajiri na msimamizi wa uchaguzi, Sylvester Masinde, akibainisha kuwa kura tatu ziliharibika.
Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baada ya Masinde kumtangaza Mbowe kuwa mshindi, idadi kubwa ya wajumbe wa mkutano mkuu walinyanyuka kwenye viti na kumfuata mbunge huyo wa Hai kwa ajili ya kumpongeza.
No comments
Post a Comment