Radi yateketeza nyumba _Ruvuma
Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limesema hali ya mvua kubwa zilizoambatana na upepo mkali na radi zimesababisha nyumba ya Mohammed Mapemba mkazi wa kijiji cha Namwinyu wilayani Tunduru kuteketea baada ya nyumba hiyo kupigwa na radi huku familia ikinusurika kutoka kwenye janga hilo kwa kuwa wote shambani.
Mvua hizo zilizoambatana na upepo zimeezua majengo ya Shule ya Msingi Mkongo ikiwemo vyumba viwili vya madarasa, stoo, nyumba na ofisi ya Mwalimu Mkuu huko wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
Aidha jiko la shule ya Msingi Mlindimila limeezuliwa huku nyumba za Wananchi takribani kumi na nane (18), nazo zikiezuliwa.
No comments
Post a Comment