Katibu Mkuu Wizara Ya Kilimo Aagiza Bodi Na Watendaji Wa Saccos Kuwasilisha Rasimu Za Taarifa Za Fedha Kwa Wakaguzi Wa Nje Coasco Kabla Ya Januari 31, 2020
Wizara ya Kilimo inawatangazia Wana SACCOS wote hasa Bodi na Watendaji wa SACCOS nchini kuwa, matakwa ya Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 (The Microfinance Act 2018), kuhusu ukaguzi wa nje ni kwamba:
SACCOS zote zinatakiwa kuhakikisha kuwa Taarifa za Fedha za Mwaka 2019 ziwe zimekaguliwa na kuwasilishwa Benki Kuu au kwa Mamlaka iliyokasimiwa ambayo ni Mrajis wa Vyama Vya Ushirika ifikapo tarehe 30 Aprili, 2020.
Kwa hiyo, Bodi na Watendaji wa SACCOS mnaagizwa kuwasilisha Rasimu za Taarifa za Fedha kwa Wakaguzi wa Nje (COASCO) kabla au ifikapo tarehe 31.01.2020 ili Ukaguzi uweze kufanyika kwa wakati na Taarifa za Ukaguzi ziwasilishwe kwa Mamlaka husika ndani ya muda uliopangwa Kisheria.
Tangazo limetolewa na:
Katibu Mkuu,
WIZARA YA KILIMO
No comments
Post a Comment