Header Ads

Header ADS

Urusi yafungiwa kushiriki michezo ikiwemo Olimpiki 2020 na kombe la dunia 2022

      Wakala wa Kimataifa wa Kupambana na Dawa za Kusisimua Misuli (WADA) limeifungia Urusi  kwa miaka minne kutoshiriki michuano mikubwa duniani ikiwemo michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao wa 2020 itakayofanyika Tokyo           Japan na Kombe la Soka la Duniani litakalofanyika nchini Qatar mwaka 2022.
Uamuzi huo unamaanisha kwamba, bendera ya Russia haitapepea wala wimbo wa taifa wa nchi hiyo hautapigwa kwenye michuano kama ya kimataifa kama ya Olimpiki ya mwaka 2020 na michuano ya kandanda ya kombe la dunia ya mwaka 2022 nchini Qatar.

  


  Pia lakini kwa wanamichezo ambao watathibitisha kutotumia dawa hizi wataruhusiwa kushiriki lakini kwa kigezo cha kutoiwakilisha Russia.

Kamati kuu ya Wada imefanya maamuzi haya katika mkutano wake mjini Lausanne, Switzerland. Hatua hii inakuja baada ya Wakala wa Kupambana na Dawa za Kusisimua Misuli nchini Urusi (RUSADA) kutajwa kutotii na kuziharibu sampuli za wanamichezo wa Russia Januari 2019.

Hata hivyo ilitakiwa kusiwasilisha sampuli hizo kwa Wakala wa Kimataifa wa Kupambana na Dawa za Kusisimua Misuli (WADA) baada ya tuhuma zilizopelekea kufungiwa kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2018.

Wada inasema kuwa, Rusada ina siku 21 za kukata rufaa. Kama haitofanya hivyo pendekezo hilo litafikishwa katika mahakama kuu ya michezo (Cas).

Licha ya kufungiwa huko, Urusi itaruhusiwa kushiriki michuano ya Euro 2020 katika jiji la St Petersburg ambao utakuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa sababu chama cha soka Ulaya UEFA hakihusiki moja kwa moja katika kesi zinazohusu dawa za kusisimua misuli.

No comments

Powered by Blogger.