Header Ads

Header ADS

Rais wa sasa wa Namibia Hage Geingob ameshinda kwa muhula wa pili

              Rais wa sasa wa Namibia Hage Geingob ameshinda kwa muhula wa pili licha ya kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya wapiga kura wanaomuunga mkono. Rais Geingob amepata  ushindi wa asilimia 56.3  ikilinganishwa na asilimia 86.7 ya mwaka 2014.

   Tume ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Umoja wa Afrika (AUEOM) imesema uchaguzi huo umefanyika kwa kufuata sheria za ndani na kukidhi vigezo vya kimataifa.Taarifa iliyotolewa  na tume hiyo imepongeza serikali na watu wa Namibia kwa kufanya uchaguzi mkuu kwa amani, na kusema uchaguzi huo uliofanyika Novemba 27 umewapatia watu wa Namibia fursa ya kuwa na uhuru wa kueleza maoni yao.Tume hiyo pia imeipongeza serikali ya Namibia kwa kuidhinisha Katiba ya Afrika kuhusu Demokrasia, Chaguzi na Utawala iliyopendekezwa na Umoja wa Afrika kufuatia uchaguzi mkuu wa mwaka 2014.Rais wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli ni miongoni mwa Marais waliotuma salamu za Pongezi kwa   Hage Geingob kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais ya Namibia kwa Muhula wa Pili, Rais wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli ni miongoni mwa Marais waliotuma salamu za Pongezi kwa   Hage Geingob kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Namibia kwa Muhula wa Pili. 

No comments

Powered by Blogger.