Header Ads

Header ADS

watu 1,221,799 sawa na asilimia 97.6 wanatumia ARV.

         Waziri Ummy amesema kuwa Vijana balehe (umri wa miaka 10 – 19) walikuwa 57,167 sawa na asilimia 4.6, na vijana (umri wa miaka 15 – 24) walikuwa 96,006 sawa na asilimia 7.7.

   Pia, amesema kati ya waliopima na kutambua afya zao watu 1,221,799 sawa na asilimia 97.6 wanatumia ARV.
Mpaka kufikia mwezi Septemba 2019 takribani watu 1,252,205 kati ya wananchi 1,600,000 wanaokadiriwa kuishi na VVU nchini walikuwa wamepima na kufahamu hali zao za maambukizi ya VVU.
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya UKIMWI duniani kitaifa yaliyofanyika jijini Mwanza.
  wanaume walikuwa 413,985 sawa na asilimia 33, na wanawake walikuwa 838,220 sawa na asilimia 77, waliopimwa na kugundulika kuwa wana maambukizi ya VVU wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU (yaani ARV’s),  
 Waziri huyo alisema wamefanya vizuri sana,”ni kuwa tumekuwa tukifuatilia kwa karibu hali za watu wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU”.Alisema
   Waziri Ummy alitaja mafanikio mengine ya kujikinga dhidi ya maambukizi ni tohara kwa wanaume ambapo kuanzia mwaka 2009 hadi Agosti 2019 jumla ya wanaume 4,456,511 wamefanyiwa tohara kupitia njia za mkoba na huduma katika vituo vya huduma
  Takwimu zinaonesha kwamba watu 953,973 sawa na asilimia 89 ya watu 1,072,650 waliopimwa wingi wa VVU wamefanikiwa kupunguza wingi wa VVU mwilini jambo ambalo ni muhimu katika kinga dhidi ya UKIMWI.Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Jamii ni chachu ya mabadiliko,tuungane kupunguza maambukizi mapya ya VVU”

No comments

Powered by Blogger.