Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wametakiwa kukamilisha miundombinu
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo leo jijini Dodoma wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa kwenye sekta ya elimu na afya wilayani Kongwa.Pia Waziri Jafo amewataka wakurugenzi hao kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi na kukiri kutokamilisha kwa wakati na taarifa hiyo iwasilishwe kwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayesimamia Elimu, Gerald Mweli kabla ya Februari 20 mwakani. Mhe Jafo amesema baada ya taarifa zao kuwasilishwa kwa Naibu Katibu Mkuu pia ziwasilishwe kwake ambapo baada ya kuipitia atatoa mapendekezo kwa Mhe Rais Dk John Magufuli juu ya wakurugenzi walioshindwa kukamilisha miradi hiyo. " Miradi hii tunaijenga mahususi kwa ajili ya kuwasaidia vijana wetu waweze kusoma katika mazingira mazuri,serikali imetoa pesa ya kutekeleza miradi hii lakini kuna baadhi ya wakurugenzi wameshindwa kusimamia utekelezaji wake,fedha zimeisha miradi haijakamilisha ilhali yapo maeneo mengine fedha hiyo hiyo miradi imekamilika na imetekelezwa kwa viwango," Amesema Jafo.Mhe Waziri amewataka Wakuu wa Wilaya wote nchini kuhakikisha wanasimamia kwa karibu wakurugenzi wao ambao hawajakamilisha miradi hiyo ili waweze kuikamilisha kwa wakati na kupeleka taarifa pia ifakapo Februari 20.Ametoa agizo kwa Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuendelea kuchunguza chanzo cha miradi ya elimu kutokamilika huku fedha zilizotolewa zikiwa zimeisha.Mhe Jafo ametoa agizo hilo alipofika katika Shule ya Sekondari ya Kongwa ambapo hakuridhishwa na namna ambavyo ujenzi wake unaendeshwa."Hapa niwaambie ukweli kwamba sijaridhishwa na utekelezaji wa miradi katika sekta ya elimu,afya mnafanya vizuri,lakini elimu hapana,fedha hizi tulizoleta ndio tumepeleka kwa wenzenu wote,iweje hapa hali iwe tofauti,lazima kuna shida hapa.Takukuru chunguzeni hapa kama upande wa manunuzi kuna shida semeni,kama kuna sehemu kuna mashimo semeni ili tujue nani amehusika kukwamisha mradi huu," Amesema Jafo.Nae Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kongwa, Abdullah Urari amesema tayari wameshaanza kufanya uchunguzi kuhusu mradi huo kwa maelelezo ya Mkuu wa Wilaya hiyo Deogratius Ndejembi aliyowahi kuyatoa."Tulichogundua katika uchunguzi wa awali hapa utaratibu wa manunuzi umekiukwa,force account haikufuatwa,walifanya makisio makubwa ya vitu na hivyo kupelekea vifaa kubaki na vitu vilinunuliwa kwa gharama kubwa," Amesema Urari.Akisoma taarifa ya ujenzi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kongwa Alex Salum alisema Januari mwaka huu walipokea kiasi cha sh milioni 290 toka wizara ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa,mabweni mawili na bwalo la chakula.Amesema mpaka sasa zaidi ya sh milioni 200 zimeshatumika ambapo ujenzi bado haujakamilika pamoja na kwamba baadhi ya vifaa vya kumalizia ujenzi huo vipo."Kwa sasa hapa ujenzi wa bwalo umefikia asilimia 75,ujenzi wa mabweni asilimia 95 na madarasa umefikia kwa asilimia 95,na matarajio yetu ni kukamilisha ujenzi huu ifikapo januari 15 mwakani," Amesema Mkuu huyo.Mbali ya kukagua miradi ya elimu katika shule mbalimbali za Wilaya hiyo, Mhe Jafo pia ametembelea Hospitali ya Wilaya hiyo Na kukagua ujenzi wa maabara, ujenzi wa chumba cha upasuaji na maabara
No comments
Post a Comment