Header Ads

Header ADS

Katibu Mkuu wa Chama cha Siasa 'Chama cha Kijamii' (CCK), Renatus Gregory Atiwa Mvaroni na TAKUKURU

     


     TAKUKURU Ilala inamshikilia Katibu Mkuu wa Chama cha Siasa 'Chama cha Kijamii' (CCK), Renatus Gregory Muabhi kwa kosa la kujifanya Mtumishi wa Serikali kutoka TAKUKURU na kuomba rushwa ya Tsh Million 50 .

Inadaiwa kiasi hicho ameomba kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya BECCO iliyopo Vingunguti Ilala Dar es Salaam.

“Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 10, 2019 majira ya jioni katika Ofisi za BECCO akiwa amepokea fedha za mtego wa rushwa Sh.Mil 1 akiwa na dhumuni la kumsaidia Manraj Bharya katika tuhuma zake zilizokuwa zinamkabili Independent Power Tanzania Limited IPTL,” amesema Mkuu wa TAKUKURU Ilala, Christopher Myava. 


Myava amesema uchunguzi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

No comments

Powered by Blogger.