Header Ads

Header ADS

Jeshi la Polisi Kigoma lazuia mkutano wa Zitto Kabwe

       Jeshi la Polisi mkoani Kigoma nchini Tanzania limezuia mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe uliopangwa kufanyika leo Ijumaa Januari 17,2020.
  Kwa mujibu barua iliyoandikwa na jana Alhamisi Januari 16, 2020 na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kigoma M.R Mayunga iliuzungumzia mkutano huo wa Zitto ikisema kutokana na mazingira ya kiusalama unapaswa kusitishwa.

“Napenda kukujulisha kuwa mkutano umezuiliwa kwa tarehe uliyoomba kwa sababu za kiusalama kutokana na taarifa za kitentejensia zilizopo. Kwa hiyo hairuhusiwi kufanya au kuendelea na maandalizi ya mkutano,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.

No comments

Powered by Blogger.