Marekani Yakiri Wanajeshi Wake 11 Walijeruhiwa na Makombora Ya Iran
Licha ya Marekani hapo awali kudai kuwa hakuna askari wake aliyeuawa au kujeruhiwa katika mashambulizi 22 ya Makombora ya Iran dhidi ya kambi mbili za kijeshi za nchi hiyo huko Iraq, lakini hivi sasa imefichuka kuwa, wanajeshi kadhaa wa Marekani walijeruhiwa vibaya na wakupelekwa kwa usafiri wa ndege katika nchi za Ujerumani na Kuwait kwa ajili ya matibabu.
Hapo jana, maafisa wa Marekani walilazimika kukiri juu ya kujeruhiwa wanajeshi wa nchi hiyo na makombora ya Iran, licha ya hapo awali kukataa kuwa kulikuwepo na majeruhi katika shambulizi hilo
Hapo jana, maafisa wa Marekani walilazimika kukiri juu ya kujeruhiwa wanajeshi wa nchi hiyo na makombora ya Iran, licha ya hapo awali kukataa kuwa kulikuwepo na majeruhi katika shambulizi hilo
Masaa machache baada ya Iran kuvurumisha makombora na kupiga kambi mbili za Marekani nchini Iraq, Rais Donald Trump alijitokeza na kudai kuwa, "Ni furaha kuwatangazia Wamarekani kuwa hakuna askari wetu hata mmoja aliyeuawa au kujeruhiwa katika shambulizi la makombora la Iran nchini Iraq."
No comments
Post a Comment