TCRA yatoa utaratibu wa kuhakiki laini Yako Ya Simu Kabla Ya Tarehe ya Mwisho January 20
Zikiwa zimebaki siku tatu laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kufungiwa, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaagiza Watanzania waliokamilisha usajili wa laini zao kuhakiki upya kwa kupiga namna *106#.
Taarifa kwa umma iliyotolewa jana Alhamisi Januari 16, 2020 na TCRA, imeeleza shughuli hiyo inapaswa kufanyika kabla ya kazi hiyo kuzima rasmi simu ambazo hazijasajiliwa Januari 20, 2020.
TCRA imesema ukomo wa Januari 20, 2020 unawahusu wale tu ambao wana laini za simu sasa (ama kwa ajili ya mawasiliano ya simu au vifaa vyao vya mawasiliano mengine) lakini hawajazisajili kwa kutumia namba ya kitambulisho cha taifa (Nida) na kuthibitishwa kwa alama za vidole.
No comments
Post a Comment