Header Ads

Header ADS

Kahama;Jamaa wa miaka 50 auawa na Mpenzi wake.

Mkazi wa Majengo mjini huko Kahama  Soko la John Maguzu (50) ameuawa kwa kupondwa tofali na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina moja la Aneth (22) mkazi wa mtaa wa Sokola kata ya Majengo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga  kutokana na kile kilichotajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
  

     Aidha kwa mujibu wa mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo John Masele amesema kuwa tukio hilo limetokea jana Alhamis Januari 16,2020 majira ya saa mbili usiku wakati Maguzu akiwa katika banda la kitimoto akipata chakula.
  "Baada ya Maguzu kumhoji mpenzi wake huyo juu ya mahusiano ya mwanaume mwingine ndipo zilipotokea purukushani na binti kumpiga mpenzi wake na tofali kichwani",aliongeza.
  Hata hivyo, Amesema kutokana na kitendo hicho Maguzu aliomba msaada kwa marafiki zake ambao walimkimbiza katika Zahanati ya Bakwata ambako alipatiwa huduma ya kwanza lakini kutokana na hali kuwa mbaya rafiki zake walikwenda Polisi na kupewa hati ya matibabu PF3 na kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama ambako mauti yalimkuta akiwa mapokezi.
George Masasi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama,  akithibitisha kupokea mwili huo amesema kuwa majira ya saa 3:30 usiku walipokea mwili wa John Masasi Maguzu (50) mkazi wa mtaa wa Sokola wilayani Kahama.
Aidha Masasi amesema kuwa uchunguzi wa madaktari umebaini kuwa ubongo ulipata hitilafu pamoja na fuvu la kichwa jambo ambalo limepelekea kifo chake na kuongeza kuwa taratibu za mazishi zinaendelea ambapo ndugu wa marehemu walieleza watasafirisha kwenda Badugu mkoani Simiyu kwa ajili ya mazishi.
    Kwa mujibu wa afisa mtendaji wa Kata ya Majengo Vicent Asenga amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo katika Kata yake na kusema kuwa alipata taarifa za tukio hilo majira ya saa nane usiku kutoka kwa viongozi wake ngazi ya mtaa huo na lushirikiana nao kumtafuta binti kwaajili ya mahojiano juu ya tukio hilo.
Kwa Maelezo ya Donald Masele ambaye ni balozi katika eneo la makazi ya Maguzu amewataka wananchi kutojihusisha na suala la mapenzi na watu wenye rika kubwa jambo ambalo linaleta madhara makubwa na kutoa ushauri kuwa wanaume wenye umri mkubwa ambao hawana wanawake waoe kuliko kutembea na mabinti wenye umri mdogo.

No comments

Powered by Blogger.