Maalim Seif na Salim Bimani watuhumiwa kufanya Mkutano bila Kibali.
Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Salim Bimani wametuhumiwa kufanya Mkutano bila kibali mnamo Desemba 2019, huko Micheweni Zanzibar
Pia, Viongozi hao wameachiwa kwa dhamana na Chama chao kupitia Mtandao wa Twitter kimedai walifanya Mkutano wa ndani usiohitaji kibali
Hata hivyo,Viongozi hao waliripoti Polisi asubuhi ya leo kuitikia wito wa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) wa Mkoa wa Kaskazini Pemba
No comments
Post a Comment