Naibu Waziri wa Nishati amesaini makubaliano ya Sekta ya Nishati ya mkutano wa Baraza na Mawaziri wa EAC
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amesaini makubaliano ya Sekta ya Nishati ya mkutano wa Baraza na Mawaziri wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Waziri ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Kikao cha makubaliano hayo hufanyika kwa njia ya mtandao(Video conference) kwa kuwakutanisha Mawaziri wa sekta husika kutoka nchi zote wanachama na kujadili masuala yanayohusu sekta ya Nishati katika kila nchi.
Hata hivyo Kikao hicho kinatokana taarifa ya Makatibu wakuu wa Wizara husika inayokuwa inazungumzia miradi ama uboreshaji wa sekta ya Nishati katika nchi hizo.
Aidha taarifa hiyo, huwasilishwa katika ngazi ya Mawaziri kwa hatua zaidi, baada ya makatibu wakuu hao kuafikiana kile walichokikusudia katika nchi zao.
Baada ya majadiliano na kuafikiana na kukubaliana kile walichokikusudia kuhusiana na sekta husika, mawaziri hao huidhinisha na kutia saini tayari kwa utekelezaji.
No comments
Post a Comment